Moja ya gari ambayo lilikuwa linabeba kokoto shuleni hapo
Wazazi wa
watoto wanaosoma shule ya msingi Lubwe iliyopo kitongoji cha Lubwe Kijiji cha
Kikota Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wamemtaka Mwalimu mkuu wa
shule hiyo Karim Msisiri kuondolewa shuleni hapo kwa tuhuma za kufuja raslimali
za shule.
Kauli hiyo
wameitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho ulioitishwa
na Mratibu wa elimu Kata Bi Tujengwe Mwangobola na kusimamiwa na Mwenyekiti wa
kijiji Godwin Mwakasege ambapo Mratibu Kata ya Ilundo Hard Mwambula alialikwa
kusikiliza.
Wazazi
walimtuhumu mwalimu Msisiri kufuja zaidi ya shilingi laki tano zilizotokana na
mauzo ya mchanga na miti ambazo ni raslimali za kijiji zilizotolewa na kijiji
kwa ajili ya kuendeleza shule hiyo lakini amekuwa akizitumia kwa matumizi
binafsi huku shule ikikosa madirisha na sakafu katika madarasa.
Akiongea kwa
niaba ya kamati ya shule hiyo mjumbe Frank Mwangomo kutokana na vitendo vya
Mwalimu mkuu kukithiri na kutoshirikisha kamati imepelekea Mwenyekiti wa kamati
ya shule Edward Kabuka kujiuzuru.
Frank
amesema kuwa kamati ya shule hiyo pia imesikitishwa na kitendo cha Mwalimu huyo
kumtumia Mwenyekiti wa kamati ya awali aliyeenguliwa ambapo mwenyekiti huyo
alitafuna pesa za shule shilingi mia moja hamsini elfu,baada ya kubanwa na
mtendaji wa kijiji Felix Michael amerejesha shilingi elfu themanini na kiasi
kilichosalia kuahidi kurejesha Februari 27 mwaka huu.
Kwa upande
wake mwalimu mkuu amekiri kufanya makosa hayo na kuomba msamaha kutokana na
majukumu mengi na kuahidi kuwa hatarudia kufanya makosa tena hivyo wazazi
wasife moyo bali waendelee kushirikiana ili kukuza taaluma kwa watoto wa shule
hiyo.
Aidha
mwalimu aliwaambia wazazi kuwa kwa
muda wa miezi saba amekusanya kiasi cha shilingi mia moja hamsini na tisa elfu
ambazo alikusanya kutokana na mauzo ya mchanga na miti na fedha hizo zilikatiwa
stakabadhi.
Baada ya
mvutano mrefu Mratibu wa Elimu
aliwataka wazazi kupiga kura kujua hatima ya mwalimu kama abaki shuleni au
la,ndipo wazai waliotaka mwalimu asamehewe walikuwa 14 na waliotaka mwalimu
aondolewe walikuwa 30.
Kwa upande
wake Mratibu aliwaambia wazazi kuwa anaheshimu mawazo yao lakini hana mamlaka
ya kumwondoa mwalimu bali atapeleka mawazo yao kwa Afisa Elimu Wilaya yeye
ndiye ana uwezo wa kutoa maamuzi lakini aliwapa muda kama watabatilisha uamuzi
wao watoe taarifa kabla ya Februari 19 mwaka huu katika mkutano watakaoitisha kupitia
kwa mwenyekiti wa kijiji.
Wakati huo
huo uchunguzi umebaini mlinzi wa shule hiyo Hamisi Mbange anadai mshahara wake
kwa kipindi mwa mwaka 2012/2013 jumla ya shilingi laki tatu na elfu ishirini na
tano ambazo hajalipwa na uongozi wa shule kwa muda mrefu bila mafanikio licha
ya wazazi kuchangia shilingi elfu moja mia mbili kwa mwaka kila mtoto.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment