Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, William
Bambanganya, anatoa wito kwa Watanzania wote walioomba kupewa hati za
kusafiria(Pasport za Tanzania) kufika ofisini kwake kuzichukua.
Amesema wasipochukua kwa muda uliotolewa
zitarudishwa makao makuu ambapo mwombaji atatakiwa kuanza upya kuomba kutokana
na hiyo ya awali kujulikana kama imepotea.
Ameyataja baadhi ya majina ya passpoti
zilizokaa muda mrefu ofisini kwake bila kuchukuliwa na kwamba wenye nazo
hawapatikani hata kwenye simu zao za mkononi kuwa ni;
1.Jonas Ngaban Hamalo
2.Twalibu Seleman Nyangasa
3.Zanya Wilson Legembo
4.Andrew Peter Pondo
5.Tadei Dominicus Pelela na
6. Christian Goden Makanyilo.
|
No comments:
Post a Comment