Ziwa Nyasa
Wananchi
wanaoishi vijiji vya pembezoni mwa
ziwa Nyasa wameiomba serikali kutatua haraka suala la usafiri wa meli ili
kutatua changamoto zinazowakabili ili kukuza pato lao na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo
wameitoa walipoongea na Mbeya yetu Blog katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Matema,Lumbila,Ifungu,Nsisi,Lupingu,Manda,Ndambi na
Lundu.
Vijiji
vingine na pamoja na Nkili,Njambe,Liuli na Mbambabay ambavyo licha ya kuwa na
fursa ya kulima na kuvua hawana uhakika wa kuuza bidhaa zao kutokana na ukosefu
wa meli ya uhakika kutokana na meli zilizopo yaani MV Iringa na MV Songea kuchakaa.
Wananc hi
hao wamesema kuwa takriblibani kwa majuma matatu meli hizo hazijafanya kazi
kutokana na kuharibika hivyo kuleta kero kwa wagonjwa mbalimbali ambao
husafirishwa kupitia njia hizo ili kwenda kutibiwa Hospitali ya Wilaya ya Kyela
au Rufaa Mbeya.
Kwa upande
wake Nahodha wa meli ya Mv Songea Thom Faya amekiri kuwepo kwa ubovu wa meli
hizo na kuiomba serikali kufanya haraka kuleta meli nyingine ili kuondoa adha
ya matengezo ya mara kwa mara ambayo hutumia fedha nyingi na wakati mwingine
huwalazimu kwenda nchi jirani ya Malawi kutokana na kukosekana cherezo.
Aidha Faya
amesema kuwa kutokana na ubovu wa mara kwa mara abiria wanahofu kupanda meli
hizo na kulazimika kuwa na abiria wachache hivyo kupata hasara kwa shirika na
kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.
Hivyo
ameiomba serikali kutimiza ahadi yake ya Rais Jakaya Kikwete ambapo aliahidi
kuleta meli mpya ili kuondoa kero inayowakabili ili kuleta msukumo wa maendeleo
kwa wakazi wa mwambao wa ziwa Nyasa ambapo njia pekee na uhakika huegemea meli.
Hivi
karibuni Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi[CCM] Abrahamani Kinana alifanya
ziara kujionea mwenyewe adha wanayopata wananchi wanaoishi pembezoni mwa ziwa
Nyasa ambapo alilazimika kusafiri na meli ya MV Songea kutoka bandari ya Mbamba
bay iliyopo wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma kupitia Mkoa wa Njombe hadi bandari
ya Itungi wilaya Kyela Mkoani Mbeya na kuahidi ombi lao kulifikisha serikalini
kwani ndiyo watekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment