Madiwani
wametakiwa kutowatuhumu watendaji wa Halmashauri au wataalamu wanaofanya kazi
Wilayani Mbozi kwa ubadhilifu bila kuwa na ushahidi wa kutosha.
Kauli hiyo
ameitoa Katibu wa Baraza Kaimu Mkurugenzi Daktari Charles Mkombachepa ambaye
amesema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa wilaya ya Mbozi
kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Januari 8 mwaka huu.
Kikao hicho
kilikuwa kinapitisha mapendekezo ya Bajeti ya Halmashauri hiyo ambapo
Halmashauri inatarajia kutumia zaidi Bilioni 44 kutokana na vyanzo mbalimbali
na wafadhili.
Mkombachepa
amesema kuwa baadhi ya waheshimiwa wamekuwa wakiwatuhumu wataalamu bila kuwa na vieelezo na ushahidi wa
kutosha na hivyo kuwavunja moyo na wengine kuamua kuomba uhamisho na hivyo
kufanya wilaya hiyo kukosa wataalamu wa kutosha.
Amesema kuwa
endapo watakuwa na ushahidi wa kutosha wawasiliane na ofisi yake itakuwa tayari
kutoa msaada ili kuleta maendeleo katika wilaya ya Mbozi.
Katika
bajeti hiyo kipaumbele kikubwa kimepewa
ujenzi wa kituo cha mabasi Mlowo kitakachogharimu shilingi milioni
600,Ununuzi wa gari la wagonjwa na gari la ukaguzi wa elimu sekondari ambapo
kila gari litagharimu shilingi milioni 150,maabara tano za shule za sekondari
zitakazo gharimu shilingi milioni 450.
Pia kikao
hicho kiliridhia kutumika shilingi milioni 95 kwa ajili ya upimaji wa mipaka
kiutawala baada ya kugawanywa kwa
wilaya za Momba na Mbozi.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Ambakisye Minga amesema kuwa makisio hayo
endapo yataridhiwa na ngazi za juu ni vema kuwa na nidhamu ya matumizi ili kila
lililokusudiwa lifanyike ili kuleta imani kwa wananchi na serikali kwa ujumla.
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment