Wananchi wa
kijiji cha Ruiwa kata ya Ruiwa wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamemgomea Diwani
wa kata hiyo Alex Mdimilaje kuchanga mchango wa ujenzi wa sekondari ya Gwili
kutokana na ubadhilifu.
Kauli hiyo
imetolewa na wananchi hao katika mkutano wa hadhara ulofanyika katika kijiji
hicho hivi karibuni kufuatia mkutano wa awali kuahirishwa wakiikataa
kamati ya elimu ya kata iliyowataka wananchi kuchangia mchango wa sekondari ya
Gwili ambapo watoto 210 wa kata hiyo kufaulu kuendelea na masomo ya kidato cha
kwanza mwaka 2014.
Wananchi hao
wamekasirishwa na kitendo cha Diwani kufumbia macho ufujaji wa pesa ambapo
wamedai kuwa jumla ya shilingi milioni 27 kudaiwa kuibwa na mhasibu wa kijiji
John Onyese ambaye ametoroka na hivi sasa anatafutwa na mwajiri wake pia jeshi
la Polisi mkoani Mbeya.
Aidha
wananchi hao wamemtuhumu aliyekuwa mtendaji kata Jordan Masweve wakidai kuwa
kwa kushirikiana na Diwani wamezorotesha maendeleleo katika kata yao huku
wananchi wakiendelea kuchangishwa michango bila kusomewa mapato na matumizi ya
sekondari kwa miaka mitatu sasa.
Pamoja na
wananchi hao kuombwa na mwenyekiti wa kijiji hicho Hadji Mohammed Dende kuwa
watulivu katika mkutano wananchi hao hawakuafiki ombi la Diwani la kutaka wachangie shilingi elfu tano
badala ya elfu kumi ili watoto waanze masomo Januari mwakani lakini wananchi
waliendelea kumzomea.
Kwa upande
wake Diwani aliendelea kuwaomba wananchi kusamehe mapungufu ya huko nyuma hivyo
warudishe moyo ili waeendelee na mchango lakini wananchi walikataa wakidai hivi
sasa hawana pesa na ni msimu wa kilimo.
Pamoja na
juhudi za Katibu kata wa chama cha Mapinduzi kata ya Ruiwa Expeditor Pius
Kibang’ole kuwaomba wananchi wakubali kuchanga walikataa wakidai hawana imani
na Diwani pamoja na kamati hivyo wapo tayari kukamatwa.
Wamesema
kuwa malalamiko yao wamefikisha kwenye ofisi ya mkurugenzi na mkuu wa wilaya ya
Mbarali lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hivyo wanamtaka mkuu wa mkoa
wa Mbeya Abbas Kandoro kutatua mgogoro huo na kuikoa kata hiyo na migogoro ya
mara kwa mara.
Mkutano huo
ulimalizika bila utaratibu wa kawaida na wananchi kumzomea Diwani huku
wakirushiana maneno makali.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment