Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, December 12, 2013

UTEUZI WA WAJUMBE WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA











 


TAARIFA KWA UMMA


UTEUZI WA WAJUMBE WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA

               Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Prof. Penina Mlama kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya. Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2005 na hati idhini ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya. Uteuzi huo ni wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10 Desemba, 2013.

               Aidha, kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza hilo, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb), Waziri mwenye dhamana ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, ambaye kwa mujibu wa hati idhini ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya na mamlaka aliyonayo amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Baraza la Chuo:

1.   Mhe. Dkt. Pindi Chana, Mbunge wa Viti Maalum-Njombe na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Sheria, Mwakilishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

2.   Eng. Peter Chisawilo, Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo, Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Mwakilishi wa Sekta Binafsi;

3.   Dkt. Haji Mwevura Haji, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, Mwakilishi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;

4.   Bw. Bernard T. D. Mbonde, Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Mwakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya;

5.   Prof. Evelyne Mbede, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia;

6.   Bw. Mapunda Erick Chrisantus, Mhadhiri na Rais wa Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Mwakilishi wa Chama cha Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya; na

7.   Bw. Augustine K. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera za Uchumi Mpana, Mwakilishi wa Wizara ya Fedha.

 Uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ni wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10 Desemba, 2013.


Imetolewa na;
Prof. Patrick J. Makungu,

Katibu Mkuu,

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.


1 comment:

Mpaju said...

SHUKURANI KWA MH RAISI, NA HONGERENI SANA NA KARIBUNI KATIKA UJENZI WA TAIFA.