Wakazi wa
jiji la mbeya wametakiwa kulinda vyanzo vya maji ili kuondokana na tatizo la
uhaba wa maji uliopo hivi sasa.
Hayo
yamesemwa na mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na mazingira jiji la mbeya
SIMIONI SHAURI alipokuwa kwenye ziara yakukagua vyanzo vya maji vya IZIWA,NSOHO
na SISIMBA.
Aidha katika
ziara hiyo Mkurugenzi huyo amesema vyanzo hivyo kwa sasa vinatoa maji kwa asilimia 87 ukilinganisha na miaka
iliyopita ambapo vilikuwa vikitoa asilimia 100
Akielezea
sababu za mabadiliko hayo amesema yamechangiwa na uharibifu wa vyanzo vya maji
ikiwa ni pamoja na kuchoma moto vyanzo hivyo na kilimo holela.
Wakati huo
huo mwana sheria wa Mamlaka ya Maji mkoani mbeya SIMONI BUKUKU amepeleka lawama
kwenye sheria za misitu kwa kushindwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya miti gani
inayofaa kupandwa karibu na vyanzo hivyo.
Katika ziara
hiyo mkurugenzi wa mamlaka ya maji mkoani mbeya aliongozana na madiwani wa kata
ya IGANZO,Mh USWEGE FULIKA na diwani wa kata ya Mwansekwa GASPER NGONELA ambapo
wameitaka mamlaka kuzidi kutoa elimu kwa wananchi wanao zunguka vyanzo vya
maji.
|
No comments:
Post a Comment