Picha ya pamoja
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)
inaendesha warsha ya Siku mbili kwa Wandaaji wa Vipindi vya Redio pamoja na
watangazaji kutoka Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, inayofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha
hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Tcra ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi,
Magreth Mnyagi amesema lengo la washa hiyo ni kuwakumbusha watangazaji kuhusu
kufuata maudhui yaliyokusudiwa yanayoelimisha na kuburudisha jamii na kuwa
chachu ya maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Amesema vipo vituo vingi ambavyo
vimekiuka maudhui yaliyokusudiwa ambayo hayazingatii maadili ya Tanzania na
kupelekea uvunjifu wa amani kutokana na kutangaza vitu vinavyokiuka maudhui
waliyopewa, hivyo kupitia Washa hiyo itasaidia kuwakumbusha kufuata misingi
taratibu na kanuni za utangazaji.
Kwa upande wake Mgeni rasmi wa Washa
hiyo, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha ambaye
alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro amesema kukiuka kwa maadili
katika baadhi ya vituo vya utangazaji kunatokana na wamiliki kuwaajiri
wafanyakazi wasiokuwa na taaluma ya Utangazaji.
Magacha amesema shida iliyopo ni kwa
wamiliki wa Vyombo vya habari ambao huajiri watu wasiokuwa na taaluma kwa
kuogopa kulipa hivyo kutafuta watangazaji wa kuokoteza ambao ndiyo chanzo cha
kukiuka Maudhui.
Aidha katika Washa hiyo washiriki
waliweza kufundishwa kuhusu Masharti na sheria ya Leseni( Licence conditions
and Code of Conduct), Kanuni za Utangazaji pamoja na kutazama DVD mbali mbali
zenye makosa kwenye vipindi vya baadhi ya Televisheni na Redio ambapo washiriki
walipata muda wa kujadili.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment