MAMBO MBALIMBALI WANAYOFANYA RAPHAEL GROUP LIMITED WASINDIKAJI WA MCHELE UYOLE MBEYA
HILI NDILO BANDA LA RAPHAEL GROUP MACHINES
MENEJA WA UZALISHAJI WA RAPHAEL MACHINES GROUP LTD, PETER D. MLEGULAH AKITOA MAELEZO YA KINA YA JINSI WANAVYOFANYA KAZI ZAO
WATUMISHI WA RAPHAEL GROUP LIMITED, KUTOKA KUSHOTO NI CHRISTOPHER MBILINYI (MUUZAJI), LAZARO MWAKIPESILE (KITENGO CHA MASOKO), PETER MLEGULAH(MENEJA WA UZALISHAJI), LUCY MWAKALAMBILE(MUUZAJI), MAMA MUSYANI(MUHASIBU)
EZEKIA WILSON(KITENGO CHA MASOKO) AKIONESHA MOJA YA BIDHAA ZA RAPHAEL GROUP
MCHELE AINA YA BROWN RICE AMBAO NI MAALUM KWA AJILI YA WATU WENYE KISUKARI AMBAO KILO MOJA INAUZWA TSH . 2000 TU
KUSHOTO NI MCHELE WA KYELA GRADE 1 NA KULIA NI MCHELE WA KAMSAMBA GRADE 1 YOTE INAUZWA TSH 1500 KWA KILO MOJA
HII NI PUMBA KWA AJILI YA MIFUGO PAMOJA NA KUTENGENEZEA NISHATI YA UMEME KILO MOJA INAUZWA TSH 50
KUSHOTO NI MCHELE WA KYELA KG 20 UNAOUZWA TSH 30,000 NA UPANDE WA KULIA NI MCHELE WA KYELA KG 10 UNAUZWA TSH 15,000
KARANGA NYEKUNDU NA NYEUPE ZINAZOINGIZWA NCHINI NA KUUZWA NA RAPHAEL GROUP LIMITED ZIKITOKEA MALAWI KWA KILO MOJA NI TSH 2000
*******
WITO umetolewa kwa serikali kuhakikisha inakuwa
karibu na Sekta binafsi ambazo zimekuwa zikijishughulisha hasa na kazi kuwainua wakulima wadogo ili kuhakikisha
wanafikia malengo yao.
Akizungumza katika viwanja vya maonyesho ya
Nanenane vya John Mwakangale jijini Mbeya Meneja wa Kampuni ya Raphael Group
Machines Ndugu Peter Mlegulah waliopo Uyole jijini hapa amesema kuwa nivema serikali sasa akizitambua
sekta binafsi katika kukuza uchumi wa Taifa .
Amesema katika Kampuni yake ambayo inahusika
zaidi na shughuli za kilimo hasa usindikaji wa mazao kwa sasa imeweza kuwasaidia wakulima zaidi ya
elfu 4 ambao wameweza kupata elimu pamoja na kukopeshwa pembejeo za Kilimo.
Amesema toka waanze shughuli hiyo wana miaka
zaidi ya 15 ambapo kazi kubwa waliyonayo ni pamoja usindikaji wa bidhaa za
Michele pamoja zao la karanga pamoja na kuwasaidia wakulima wadogo ili waweze
kufikia malengo yao hasa kwa kuwapatia elimu ya kilimo na ushauriwa kitaalam.
Amesema wakulima walio wawezesha wameweza
kuondokana na kilimo cha kienyeji ambapo kwa sasa wakulima hao wameweza kuinuka
kwa kuongeza uzalishaji toka gunia 40 hadi gunia 80 kwa Hekta, hivyo kampuni
hiyo imekuwa mkombozi mkubwa kwa
wakulima wa Kanda ya Nyanda za juu kusini.
Amesema
malengo yao ni kuwafikia wakulima zaidi ya Laki moja(100,000) ili kuhakikisha
wanaisadia serikali katika kupunguza tatizo la ajira nchini kwa kudhibiti idadi
kubwa ya vijana wanao toka vijijini na kukimbilia mijini.
WASILIANA NAO SASA KUPTIA SIMU NAMBA +255 784 409340 NA +255 767 409340
BARUA PEPE: info@.rafagrouplimited.com / pmlegulah@yahoo.com
TEMBELEA WEBSITE YAO: www.rafagrouplimited.com
1 comment:
kazi nzuri mpaka raha
Post a Comment