JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO
WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA
(PSPF)
UHAKIKI
WA WASTAAFU NA WATEGEMEZI
Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unawakumbusha wastaafu na wategemezi
wanaolipwa pensheni na Mfuko huu kufika na kujihakiki katika Ofisi za PSPF zilizopo
katika Makao Makuu ya Mkoa uliyopo.
Mstaafu au mtegemezi anatakiwa kujihakiki kila baada ya miezi sita yaani
Januari na Julai.
Fika
kujihakiki ukiwa na nyaraka zifuatazo:
1.
Kitambulisho cha mstaafu au mtegemezi
au kadi ya mpiga kura (endapo hujapatiwa kitambulisho),
2.
Kadi ya benki unayopokelea pensheni,
3.
Picha moja ndogo ya rangi (passport
size)
Wastaafu
na Wategemezi waliopo Zanzibar watahakikiwa tarehe 1-3 Julai 2013 Makao Makuu
ya Polisi (Ziwani) Unguja na tarehe 4-5 Julai 2013 ofisi za Polisi Chake Pemba.
Kutojihakiki kwa muda unaotakiwa kutasababisha malipo yako ya pensheni
kusitishwa bila taarifa.
“PSPF TULIZO LA WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi
wa Umma,
No comments:
Post a Comment