SERIKALI imeendelea kuchukua hatua za
kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatumika kama zilivyokusudiwa kwa ustawi
wa maendeleo ya nchi na wananchi wake.
Moja ya hatua ambazo serikali imechukua ni
pamoja na kuanzisha Idara ya Mkaguzi wa ndani mkuu wa serikali ambayo imepewa
jukumu la kusimamia ,kueindeleza na kuboresha huduma zaukaguzi wa
ndani katika serikali na kuwaendeleza kitaaluma wakaguzi wa ndani.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mbeya na Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa mbeya Ndugu Nicolausi Ntangu wakati wa ufunguzi wa semina
ya wadau wa ukaguzi wa ndani kanda ya nyanda za juu kusini iliyo fanyika
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mkapa.
Kaimu Katibu Tawala huyo amesema kuwa ofisi ya
mkaguzi wa ndani inasaidia kwa asilimia kubwa katika kusimamia utawala
bora hasa katika mamlaka za serikali mitaa.
Amesema pia idara hiyo imekuwa ikihusika
mojakwamoja katika usimamiaji na uwajibikaji wa matumizi bora
ya rasilimali za umma kama inavyoshauriwa kupitia taarifa mbalimali za ukaguzi
wa ndani hivyo dhana ya uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali umma kuwa
muhimu sana kwa utendaji wa serikali.
Hata hivyo Ntangu amesema kuwa kumekuwepo na
baadhi ya vitendo vinavyo fanywa na baadhi ya watendaji katika halimashauri na
menejmenti mbalimbali nchini ambao umekuwa ukiwakwamisha wakaguzi wa ndani
katika kutekeleza majukumu yao .
Amesema kuwa nivyema vitendo hivyo vya
ukandamizwaji kwa wakaguzi wa ndani vikakoma kwa lengo la
kuhakikisha ukaguzi wa ndani unapewa rasilimali za kutosha na kupewa
kipaumbele katika utendaji wao wa kazi za kila siku.
Pia katibu tawala huyo amefafanua kuwa ili
kuhakikisha Idara za ukaguzi wa ndani zinafanya kazi zake kwa weledi nivema M
ameya ,Wenyeviti wa halimashauri na Wenyeviti wa kamati za ukaguzi wa za
halimashauri kuhakikisha zinatoa fursa kwa wakaguzi hao wa ndani ili
waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo katika usimamizi wa rasilimali za
nchi.
Hata hivyo kwa upende wake Mkaguzi wa
Ndani wa Serikali Msaidizi Ndugu Chetto Sendo amesema semina hiyo ni sehemu ya
mkakati wa Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa serikali wa kuimalisha mfumo
wa uwajibikaji na utawala bora katika matumizi ya rasilimali za
umma chini ya program ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma awamu ya nne(
PFMRP IV).
Amesema semina hiyo pia itasaidia kuamsha
hamasa kwa watendaji wa halimashauri kwa lengo la kuanza kuona
ukaguzi ndani kama kiungo muhimu katika utekelezaji wa majukumu kama kiungo
muhimu katika utekelezaji wa majukumu na kufikia malengo.
Amesema semina hiyo inatalajiwa kufanyika
katika kanda zingine za kati ,kaskazini ,ziwa na mashariki kwa
kushirikisha makundi yote katika halimashari zitakazo husika.
Na Mbeya yetu
|
1 comment:
Editor Mbeyayetu proof reading ni nzuri kabla ya kuweka habari, mfano Halmashauri umeandika HALIMASHARI, inaharibu maana
Post a Comment