Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, June 13, 2013

MSHIKEMSHIKE wa Jina la Mkoa Mpya utakaogawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya umezidi kushika kasi baada ya kila pande kupendekeza majina kutokana na maeneo wanayotoka.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi Ambakisye Minga Alisema hali ya miundombinu ni nzuri katika kila Wilaya zilizopendekezwa na kwamba Wilaya ya Chunya  igawanywe kufuata majimbo ya Uchaguzi kwa Jimbo la Lupa liwe Mkoa wa Mbeya na Songwe kuwa mkoa wa Songwe.

Mkuu huyo wa Wilaya Dk. Kadeghe alitumia Fursa kupiga marufuku uuzaji na ununuaji wa kahawa mbichi maarufu kwa jina la Cherry Wilayani humo kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara kuanza kuwarubuni wakulima.
Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Elisey Ngoyi alitoa taarifa hiyo huku akitaja Wilaya zitakazounda Mkoa Mpya kuwa ni Mbozi, Momba, Ileje, Chunya, Mbalizi na Igamba ambazo zote zinapitiwa na Mto Songwe.








MSHIKEMSHIKE wa Jina la Mkoa Mpya utakaogawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya umezidi kushika kasi baada ya kila pande kupendekeza majina kutokana na maeneo wanayotoka.

Sakata hilo limetokea hivi karibuni baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba wakitaka Mkoa huo kuitwa jina la Momba huku Wilaya ya Mbozi ikipendekeza Mkoa Mpya uitwe Songwe.

Wakizungumza katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo walisema sababu ya kuitwa kwa Songwe kunatokana na Mto Songwe kupitia Wilaya zote ambazo zitaunda Mkoa Mpya.

Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Elisey Ngoyi alitoa taarifa hiyo huku akitaja Wilaya zitakazounda Mkoa Mpya kuwa ni Mbozi, Momba, Ileje, Chunya, Mbalizi na Igamba ambazo zote zinapitiwa na Mto Songwe.

Pia alipendekeza Makao makuu ya Mkoa huo kuwa Tarafa ya Vwawa Wilayani Mbozi kwa kile alichodai kuwa ni katikati ya Wilaya Zote hali itakayowarahisishia wananchi kutembea kwa muda mfupi kutoka Kila Wilaya.

Kauli hiyo pia iliungwa mkono na Baraza zima la Madiwani chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ambakisye Minga walisema hali ya miundombinu ni nzuri katika kila Wilaya zilizopendekezwa na kwamba Wilaya ya Chunya  igawanywe kufuata majimbo ya Uchaguzi kwa Jimbo la Lupa liwe Mkoa wa Mbeya na Songwe kuwa mkoa wa Songwe.

Waliongeza kuwa katika Wilaya hizo zinashabihiana katika mambo mengi yakiwemo Shughuli za kiuchumi , utamaduni , uoto wa asili, ukubwa Kijografia na mazao ya kilimo ambayo hulimwa na kustawi katika Wilaya kama vile Kahawa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbozi, Charles Mkombachepa aliwashukuru madiwani kwa michango yao na kwamba Mchakato huo utapelekwa katika Baraza la Ushauri la Wilaya kwa ajili ya kujadiliwa na kupelekwa baraza la Mkoa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Dk. Michael Kadeghe aliwataka wajumbe watakaohudhuria Baraza la Ushauri kusimamia maamuzi yaliyopendekezwa na madiwani yasije yakabadilishwa na kuwakosesha raha wananchi kwa mawazo yao kupitia wawakilishi wao ambao ni madiwani.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Wilaya Dk. Kadeghe alitumia Fursa kupiga marufuku uuzaji na ununuaji wa kahawa mbichi maarufu kwa jina la Cherry Wilayani humo kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara kuanza kuwarubuni wakulima.

Alisema wakulima hao hurubuniwa kwa kuuza kahawa hiyo kwa bei ya chini hali ambayo inadidimiza uchumi na kwamba hali hiyo hataivumilia katika Wilaya yake na kuongeza kuwa kwa atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Picha na E. Kamanga
Mbeya yetu

No comments: