Mnyukano wa ugawaji wa
mkoa wa Mbeya umeendelea kujenga sura ya uasilia wa waliopo kwenye madaraka
kutokana na wanasiasa kuvutia maeneo walikotoka bila kujali vigezo vya msingi
ikiwemo idadi ya watu.
Kulingana na vikao
vinavyoendelea, wilaya ya Rungwe tayari imeshajitengenezea mazingira mazuri ya
kupigiwa debe kuwa mkoa kwa kile kinachobainishwa kuwa madiwani wengi katika
mkoa wa Mbeya asili yao ni wilaya ya Rungwe
Dhana ya “kumitu
kukhaja ” inaonekana wazi wakati huu kwenye mchakato wa kutoa mapendekezo
ya wapi na maeneo yapi yaunganishwe kuunda mkoa wa mpya baada ya Mh Rais
Kikwete kutamka wazi na kubariki mchakato huo wakati wa maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi mei mosi.
Mfano wa kujipigia debe
unaonyesha kuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbarali Keneth Ndingo ni mkazi wa
Rungwe hivyo maamuzi ya baraza la madiwani la Mbarali yanaonekana kuwa na
msukumo wa nyumbani, ambapo wamependekeza makao makuu yawe Rungwe
Maajabu ya musa
yanajitokeza katika ugawaji unaopendekezwa ambapo inaelezwa kuwa Mbarali wanapendekeza
halmashauri za Busokelo, Rungwe, Kyela, Ileje na Mbozi ziunde mkoa mpya wakati
kijiografia havina uwiano kati ya Mbozi na Rungwe.
Kulingana na takwimu za
sense ya mwaka2012, wilaya ya Mbozi kabla ya kugawanywa kupata Momba ilikuwa na
wakazi 740,719 idadi ambayo ni sawa na idadi za wakazi wa wilaya za Kyela,
Rungwe na Ileje ambazo kwa pamoja ni wakazi 685,098 hivyo kuwepo kwa pengo la
55621 zaidi kwa upande wa Mbozi
Kulingana na jiografia
ya mkoa wa Mbeya, Mkoa ambao kwa sasa ungeweza kuundwa kwa kuunganisha wilaya
za Ileje, Mbozi, Momba na sehemu ya wilaya ya Chunya (jimbo
la Songwe) ambalo limejitenga na eneo la Lupa kwa umbali wake.
Kwa takwimu hizo hizo
mkoa wa huo ungeweza kuwa na idadi ya wakazi 1,201,327 ambao ni
asilimia 44.4 ya takwimu za sasa za wakazi wa mkoa wa Mbeya wanaofikia
2,707,410.
Ingawa jitihada za
kujipanga zimeanza kwa upande wa wilaya za Rungwe, Mbarali na Kyela kwa kufanya
ushawishi wa mbinu,ukweli unabakia kuwa wilaya ya Mbozi peke yake inavigezo
vyote vya kupata mkoa mpya kuanzia idadi ya watu, eneo la utawala,makazi, uwezo
wa raslimali za ndani kujiendesha na fulsa za kiuchumi zilizopo na zinazoweza
kupatikana.
|
1 comment:
Taarifa kama hizi zinachochea ubaguzi katika jamii. Aache siasa huyu kwani nani asiyependa kwake, yeye mwenyewe anaonekana anatokea huko anakotaka mkoa uende.
Post a Comment