askari WDR Ambrose akitinga mahakani kusikiliza hukumu ya watuhumiwa wake
Watu wanne wamefikishwa Mahakamani
wakituhumiwa kutenda kosa la kufanya unyang’anyi wa kutumia Silaha kwa kumpora
Askari Magereza Bunduki na hukumu ikitolewa kwa Mshtakiwa mmoja ambaye
amehukumiwa miaka 30 jela.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali Mwajabu Tengeneza
akisoma Mashtaka Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya Aneth
Nyenyema amesema Washtakiwa wote wanne kwa pamoja walitenda kosa hilo
kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 287(A) sura ya 16
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Amewataja watuhumiwa kuwa ni Ali Salum (32)
ambaye ni mshtakiwa namba moja akiwa na Emmanuel Martin(25), Braison Sanga na
John Waziri(22) ambao ilidaiwa kuwa Mei 5, Mwaka katika eneo la Magereza Songwe
walimvizia askari WDR Ambrose na kumjeruhi kisha kumpokonya bunduki aina ya SRA
yenye namba za usajili TZ PS 39847164020 mali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kitengo cha Jeshi la Magereza.
Kutokana na Mashtaka hayo watuhumiwa wote
walikana isipokuwa Mshtakiwa namba moja ambaye alikubali kutenda kosa hilo hali
iliyomlazimu Mwendesha mashtaka kumsomea mara tatu ili kujua kama ameelewa
mashtaka yake.
Na Mbeya yetu
|
1 comment:
silaha siyo siraha ndungu yetu, kiswahili ni lugha yako.
Post a Comment