Add caption
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kata ya Iyela Jiji la
Mbeya kimewaahidi wanachama na wananchi wake kutekeleza na kuyaendeleza
mambo mazuri yaliyoachwa na viongozi waliopita ili kujenga imani na Serikali
yao ya Chama.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Richard, Shangwi wakati wa hafla ya Uchukuaji wa Fomu ya kugombea Udiwani katika kata ya Iyela
kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa kata hiyo, Dominick Tweve aliyekuwa
maarufu kwa Jina la Mzee Nkwenzuru aliyefariki dunia Mwaka jana Agosti 9,
Hafla iliyofanyika katika Ofisi za Afisa Mtendaji wa kata hiyo.
Richard alisema Chama chake kimemwamini na
kumpendekeza yeye kuwania Udiwani ili akayaendeleze mazuri yaliyofanywa na
Diwani aliyepita sambamba na mengine aliyokuwa ameanza kuyafanya na kuishia
njiani kabla ya kufikwa na Umauti.
Katika uchukuaji wa Fomu hiyo Richard Shangwi alisindikizwa na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwemo viongozi mbali mbali
kama Mwenyekiti wa Chama Wilaya, Katibu Mwenezi Mkoa, Katibu wa UVCCM Mkoa,
Ktibu wa Chama Wilaya, Katibu Mwenezi wa Wilaya, Mnec, Mjumbe wa Mkutano mkuu
taifa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Fomu hizo,
Mgombea huyo alisema kama Chama wanategemea kurudisha Fomu Mei 13, Mwaka huu
majira ya Saa tano asubuhi ambapo Kampeni kwa ajili ya kunadi Sera za Chama
zitazinduliwa Mei 18, Mwaka huu na kutumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kufika
kwa wingi katika Mikutano ya Kampeni itakapoanza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa kata
hiyo ambaye pia ni Afisa Mtendaji wa kata ya Iyela Safi Almasi alisema zoezi la
uchukuaji Fomu lilianza kwa kusuasua ambapo rasmi wameanza kuchukua Mei 9,
Mwaka huu zoezi ambalo litafikia ukomo Mei 12, Mwaka huu.
Mtendaji huyo aliwataja wagombea waliojitokeza
kuchukua Fomu ni kutoka chama cha DP Amos Anyisile Mwambagi,
kutoka CHADEMA Charles Changani Mkera na Mgombea wa Chama cha Maapinduzi
Shangui J. Richard.
Aliongeza kuwa Wananchi kutoka Vyama vyote vya
Siasa wajitokleze kuchukua Fomu hizo ili kuendana na muda waliopangiwa
kuendesha zoezi la Uchaguzi huo na kuongeza kuwa Kampeni zitaanza Mei 15, Mwaka
huu wakati zoezi la uchaguzi na upigaji kura litafanyika Juni 16, Mwaka huu.
Na Mbeya yetu
|
1 comment:
Kila la kheri Kaka, ila kwa chama ulikopitia mmhh
Post a Comment