Hoteli ya Golden City ya Jijini Mbeya.
Chama Cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA)
kimeendesha mafunzo kwa wanachama wake 81 ambao wanatoka katika Majimbo 27 ya
Uchaguzi katika Kanda ya Nyanda za Juu kusini Mafunzo yanayofanyika Katika
Ukumbi wa Hoteli ya Golden City ya Jijini Mbeya.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Organaizesheni wa
Chadema Taifa Singo Bensoni alisema Lengo la Mafunzo hayo ni kuhakikisha
wanapata wakufunzi 30606 nchi nzima ambao watatawanyika katika kila kitongoji
nchi nzima kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi na kuunda matawi ya Chama
hicho ikiwa ni pamoja na kukifikishama hadi ngazi ya Chini.
Alisema mafunzo hayo yalianza kutolewa kwa
kuchukua wakilishi watatu kila Jimbo la Uchaguzi ambao baada ya kumaliza
watafanya mitihani na kufuzu kuwa wakufunzi wa chama na kuongeza kuwa mbinu
itakayotumika ni kuendesha mafunzo ya chini kwa chini bila kuvaa sare za chama
wa kutumia magari ya matangazo na vipaza sauti.
Aliongeza kuwa katika mafunzo hayo yanahusisha
wawakilishi wawili kila kanda ambao waliungana na wanachama wengine 10 wa
Kitaifa ambao jumla walikuwa 30 ambao baada ya kufuzu mafunzo walirudi
kufundisha katika kanda zao ambapo katika Kanda ya Mbeya ina wanafunzi
81,Arusha 96, Mwanza 72 na Shinyanga 60 ambao wanawakilishwa na watu watatu
kila Jimbo la Uchaguzi.
Aidha alisema mafunzo hayo yanatolewa kutokana na
ufadhili wa watu wa Ujerumani na kwamba wakufunzi hao watapewa Miezi miwili
kuhakikisha wameyafikia maeneo yote nchini na kufanikiwa kuwapa elimu wananchi
wapatao 30 kwa Mtu mmoja na kuunda Msingi tayari kwa maandalizi ya Uchaguzi
mkuu ujao.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment