IMEELEZWA kuwa Uuguzi na Ukunga ni taaluma muhimu
yenye mchango mkubwa katika kuboresha huduma za Afya nchini, ambapo wametakiwa
kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, taratibu na miongozo ya kazi
zao.
Aidha wauguzi na wakunga wametakiwa kufuata
miongozo ya kitaaluma iliyowekwa na kuthamini, kuheshimu uhai wa wa watejwa
ambao ni wagonjwa bila kujali uchumi wa mtu, rangi, kabila au ugonjwa alionao
kwa kuongozwa na misingi ya maadili ya Uuguzi na Ukunga.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Afya Mkoa wa Mbeya,
Juliana Mawala katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyka katika hospilatali ya mkoa alisema Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka imekuja katika muda
mwafaka ambayo inasema “Kuziba Mapengo kufikia malengo ya millenia
namba 4,5 na 6.”
Mawalla alisema kuwa dunia ipo kwanye
mapambano dhidi ya vifo vya mama na Mtoto vitokanavyo na sababu ambazo zinaweza
kuzuilika endapo wauguzi watajikita zaidi katika kutekeleza maazimio ya malengo
ya milenia zilizotajwa.
Alisema maadili ya Uuguzi ndiyo dira na
Mwongozo wa dhana ya uuguzi kwa wauguzi wote nchini ,Hivyo mnapaswa kuzingatia
maadili ya Uuguzi, huku mkitekeleza maagizo ya sera na Miongozo
mbalimbali itolewayo na Baraza la Uuguzi na Ukunga pamoja na Wizara ya Afya na
Ustawi wa jamii.
Aidha Katibu huyo alikili uwepo wa wauguzi
wachache ambao wamekuwa na tabia ndogondo zisizoendana na Maadili ya
Uuguzi, ambapo alitoa wito kwa Wauguzi kushirikiana kuwakemea na kuwafichua
pale inaposhindika ili wauguzi hao wachache wasiharibu Fani hii nzuri ya
Uuguzi.
Pia aliwaasa wauguzi kutekeleza wajibu wake katika
kupambana na Janga la Ukimwi na kuongeza kuwa wasipime Virusi Vya Ukimwai
kwa macho na kudhani kuwa mtu mwenye Afya Nzuri hajaambukizwa bali watumie
vipimo vilivyodhibitishwa kitaalamu.
“Ndugu Wauguzi , napenda kuwahamasisha na
kuwasisitiza juu ya umuhimu wa kuwa kitu kimoja na kushirikiana katika
kuboresha na kukuza chama chenu kwa kuhakikisha kuwa kila muuguzi ni mwanachama
na anashirikiana na wenzake katika michango mbalimbali kwani mahali penye chama
ndipo panapoweza kuwaunganisha watu na wakaweza kuwa na nguvu ya kuongea kwa
kauli moja , hivyo viongozi lisimamieni hilo nasisi tunaahidi
tutakuwa pamoja nanyi ii kuhakikisha chama chenu kinakuwa imara”
alisisitiza Katibu huyo.
Aliongeza kuwa katika huduma za afya
apewazo mgonjwa, Muuguzi hutoa theluthi mbili ya huduma zote azipatazo
mgonjwa na tunakiri kuwa Hospitali bila Muuguzi haitaweza kuitwa
hospitali hivyo basi kuweni mifano bora katika utoaji wa huduma za Afya,
kuweni wabunifu Muwahudumiapo wagonjwa na kuweni watetezi na washauri wa
wataalamu wengine katika kumhudumia mgonjwa.
Na mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment