Baadhi ya wakazi wa Iyunga walishuhudia tukio hilo
Wito umetolewa kwa wadau mbalimbali na wananchi
mkoani mbeya kuhakikisha wanatoa michango yao katika kuhakikisha jeshi la
polisi linaendelea kuimalisha ulinzi na usalama kwa jamii.
Michango hiyo ni pamoja na kujenga vituo vya
Polisi na ukarabati ambao utaweza kutoa fursa kwajeshi hilo kufanya kazi kwa
bidii katikakuhakikisha jamii inaendelea kuishi maeneo salama na tulivu.
Akizungumza katika makabidhiano ya kituo cha
polisi Iyunga jijini Mbeya Ndugu Haji Ally Promosheni Meneja kutoka
Kampuni vinywaji baridi ya Coca cola ambayo imefadhili ukarabati wa kituo
hicho kilicho gharimu kiasi cha shilingi milioni 10 amesema wao kama kampuni
wametoa msaada huo kwa lengo kurudisha kile walicho kipata ndani ya jamii.
Amesema yapo maeneo mbalaimbali ambayo wameweza
kusaidia jamii hasa katika sekta ya elimu .afya pamoja na maeneo mengine
hivyo kitendo cha wao kusaidia jeshi hilo la polisi ni kama muendelezo wa
matukio yanayo fanywa na kampuni hiyo .
Meneja huyo ameyataka mashirika
mbalimbali mkoani humu kuhakikisha wanasaidia maeneo yanayo hitaji misaada kama
ambavyo wao wameweza kuonyesha mfano kwa kukarabati kituo hicho cha Iyunga
ambacho awali kilikuwa katika hali mbaya.
Amebainisha kuwa msaada huo haujaishi kwa jeshi
la polisi pekee kwani bado kuna maombi mbalimbali ndani ya jamii ambayo
yanahitahi kupatiwa misaada kutoka katika kampuni hiyo hivyo ameahidi kuendelea
kutoa ushirikiano wao katika kuijenga jamii ya mkoa wa mbeya.
Kwa uapande wake kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Barakaeli Masaki ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao katika
kuimlaisha ulinzi na usalama katika jiji la mbeya.
Amesema mchangho ulio tolewa na Kampuni hiyo ni
mkubwa kwani umeweza kuboresha mazingira bora ya kituo hicho na kulifanya jeshi
hilo kufanya kazi zake kwa usanifu.
Pia amezitaka taasisi mbalimbali pamoja na
mashirika mengine kuendelea kutoa michango yao kwa jeshi la polisi mkoani humo
ikiwa ni pamoja na kuimalisha vituo vingine vya polisi ambavyo hali yake
hairidhishi.
Picha na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment