Hawa Mathias,Mbeya.
BAADHI ya wananchi wanaotumia vyombo vya usafiri maarufu (daladala) Mkoani Mbeya wameomba mamlaka ya usafirishaji wa nchi kavu na majini (SUMATRA) kushirikiana na jeshi la polisi kufanya ukaguzi wa haraka wa magari mabovu ili kuweza kuthibiti ajari za barabarani zinazochangiwa na ubovu wa vyombo vya usafiri.
Wakizungumza na Mwananchi baadhi ya wananchi wanaosafiri kati Sokomatola kwenda uyole na sokomatola Mbarizi wamesema kuwa vyombo vingi vya usafiri havina sifa ya kusafirisha abiria na badala yake wamiliki wamekuwa wakitanguliza maslai ya fedha badala ya uhai wa abiria na mali zao.
"Ifikie wakati idara husika kusimamia hilo na kusikiliza kero za wananchi na na kuwataka askari wa jeshi la polisi kitengo cha usalma barabarani kutojenga mazoea na madereva na makondakta na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia maadili na kanuni za kisdheria ili kukabiliana na hali hiyo ili kuthibi hali ya usalama barabarani "Alisema Jordan Mwaisanila mkazi wa uyole
"Tunaomba sumatra kushirikiana na jeshi la polisi na umoja wa chama cha madereva ili kuweza kukaa pamoja na kujua nini cha kufanya ili kuthibiti hali hii kwani mabasi mengi ni mabovu na madereva wengi wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani kwa kuendesha magari kwa mwendo kasi,kutovaa sare na kutoa lugha chafu kwa abiria"Walisema.
Naye Mkazi wa Mji mdogo wa mbarizi Selina Jonhson alisema kuwa sasa ifikie wakati jeshi la polisi kitengo cha usalama barabani kuweka mikakati kabambe ili kuhakikisha linaendesha zoezi kwa kuzingatia kanuni na sheria na kutomuonea kwa kutoza faini kubwa ili kuweza kutoa fundisho kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri waweze kutambua wajibu wao wa kuvifanyia matengenezo vyombo vya usafiri na si kutanguliza masli ya fedha mbele.
"Sasa ifikie wakati hata polisi wa usalama barabarani akufanya ukaguzi wa magari na kufanya mazoea na madereva na makondakta na hivyo ni jukumu lenu kutambua nini kinachowaweka barabarani kwani kukagua leseni na mataili bado hamjatambua ubovu wa vyombo vya usafiri"Alisema Jordan Mwasakyeni.
Johnson alisema kuwa wamiliki wa vyombo vya usalama wanapaswa kutambua majukumu yao kwa watazania kwa kufanya ukarabati na matengenezo ili kuepuka hasara na vifo vya wananchi vinavyotokana na ajari za barabarani.
No comments:
Post a Comment