Na Esther Macha, Mbeya
KUFUATIA wizi wa mita za maji kukifiri Mkoani Mbeya Mamlaka ya maji imesema kutokana na kutambua umuhimu wa huduma hiyo wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo kwa mtu yeyote ambaye anajihusisha na wizi wa mita hizo ambazo zimekuwa zikiingizia hasara mamlaka.
Akizungumza na majira ofisini kwake jana Ofisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bibi.Neema Stanton alisema tatizo hilo ni kubwa kwa mamlaka la wizi wa wizi ambalo si zuri na linakwamisha utendaji wa kazi wa kila siku.
“Maeneo yote ya Jijini mbeya tunaomba wananchi watoe ushirikiano wa dhati wa kuhakikisha suala hili la wizi wa mita linakwisha hivyo wananchi watumie namba hii kutoa taarifa ambayo ni 0800755533 ili kuweza kuwabaini watu hawa”alisema.
Akizungumzia kuhusu maeneo ambayo yanaibwa mita alisema ni Kata ya Ilemi,Iganzo,Isanga hizi kwa ujumla ndo zimekuwa na matatizo ya kuibwa mita mara kwa mara katika maeneo yao.
Bibi.Stanton alisema kuhusu wizi wanaendelea na uchunguzi kujua mita hizo baada ya kuibwa zinafanyiwa nini na kuwafahamu wahusika wakuu ili waweze kuchukuliwa hatua haraka kutoklana na wizi huo.
Hata hivyo alitaja idadi ya mita zilizoibwa kuwa ni zaidi ya 300 ambazo zimelipotiwa kiofisi na kuongeza kuwa hasara ambayo wanaipata mara baada ya mita hizo kuibwa ni upotevu wa maji ambayo hutiririka muda wote kutokana na kuwa wazi.
Akizungumzia hasara ambayo mamlaka inapata alisema baada ya mita hizo kupotea alisema ni kununua mita zingine licha ya kuwa wateja huchangia kiasi Fulani bado inaleta hasara kwa mamlaka.
No comments:
Post a Comment