Mkurugenzi wa jiji la mbeya Juma Idi akiongea na waandishi wa habari Joseph Mwaisango wa mbeya yetu Hosea Cheyo wa TBC na Chales Mwakipesile wa gazeti la majira
HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, inatarajia kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 1.7 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kuishi na kufanyia kazi watumishi wake pamoja na kuongeza vitendea kazi.
Akizungumza na Mbeya yetu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Juma Iddi, alisema halmashauri ya jiji imeandaa mpango wa muda mrefu wa kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wakazi wake.
Alisema, moja ya mikakati iliyobuniwa ni kuboresha mazingira ya kuishi na kufanyia kazi watumishi, sambamba na kuboresha uwezo wao wa kutenda kazi kinyenzo kwa kuongeza vitendea kazi muhimu.
Alisema, chini ya mpango huo jumla ya nyumba 10 na ofisi 12 zitajengwa katika kipindi cha miaka 5 kuanzia 2011/12 na jumla ya magari 24(12 kwa ufadhili wa mradi wa TSCP).
Pia, alisema jumla ya pikipiki 120, kijiko kidogo, wheel Loader moja ambavyo vyote vitanunuliwa ndani ya kipindi hicho.
Aidha, alisema kuwa mpaka sasa halmashauri imefanikiwa kununua magari 2 kwa milioni 85, pikipiki 36 kwa shilingi ya milioni 82.
Alisema, tayari imeagiza na kulipia kwa fedha zake magari 3 ya utawala likiwemo la afya, Ambulance na idara ya sheria ambayo yatawasili muda wowote ambapo gharama halisi itafahamika mara ya kuwasili kwa kuwa itajumlisha Bima na usafirishaji.
Alisema, ujenzi wa jingo la ghorofa 2 katika ofisi kuu utaanza muda mfupi baada ya taratibu za zabuni kukamilika ambapo ujenzi huo unatarajia kutumia milioni 800.
Hata hivyo alisema halmashauri inajenga nyumba moja ya mkurugenzi wa Jiji sambamba na kukarabati nyumba 2 za wakuu wa idara.
No comments:
Post a Comment