Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, December 4, 2011

ASILIMIA 80 YA MAWAKALA WILAYANI MBOZI MBEYA WAGOMA BAADA YA KUTOLIPWA.

Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gabriel Kimoro akihutubia wananchi wilayani kwake.
Mwenyekiti  wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Minga Ambakisye.

Asilimia 80 ya mawakala waliotakiwa kusambaza pembejeo za ruzuku wilayani Mboai mkoani Mbeya wamegoma kutokana na kutolipwa fedha zao za msimu uliopita 2010-2011.

Hayo yamebainika siku chache baada ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kuwaeleza Maaskofu, Wachunga na wanataaluma wa mkoa wa Mbeya kuwa mkoa umepata pembejeo za kutosha ambapo mawakala 350 walikuwa tayari wamechaguliwa kuzisambaza katika wilaya zote nane zilizopo mkoani hapa.
 
Kondoro aliyasema hayo katika mkutano wa pamoja katika kanisa la Winners Jijini hapa wakati wa kujadili mafanikio na changamoto za maendeleo ya mkoa tangu uhuru wa Tanganyika.

Baadhi ya mawakala ambao wamegomea zoezi hilo la usambazaji wa pembejeo hizo wilayani Mbozi walisema kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya kuingia hasara kubwa ya kutolipwa na Serikali baada ya zoezi la kusambaza pembejeo hilo kumalizika.

Walisema kwa msimu huo uliopita, mawakala wengi mpaka sasa wanaidai Serikali zaidi ya Milioni 40 ambazo mpaka sasa hawajalipwa huku Serikali ikiwataka waingie tena kwenye mkataba mpya wa kuto fedha zao huku wakiwa hawana uhakika wa kulipwa baada ya kumaliza zoezi hilo.

Mmoja wa mawakala hao Japhari Masebo alisema kutokana na jambo hilo wameiomba Serikali ya wilaya hiyo kuwalipa fedha zao au kabla ya kulipwa na kusambaza pembejeo hizo kwa msimu huu  wa mwaka 2011-2012 kusainiana mikataba ya kulipwa baada ya zoezi jambo ambalo Serikali imegoma.

Hali hiyo imeyatisha hata makampuni binafsi yanayojihusisha na kilimo yaliyokuwa tayari kusambaza pembejeo hizo kwa bei nafuu ikiwemo kampuni ya Lima inayojihusisha na ununuzi na usindikaji wa kahawa wilayani humo.

Meneja wa kampuni hiyo Tinson Nzunda alisema kuwa kampuni yake ipo tayari kusambaza pembejeo hizo lakini mpaka pale Serikali itakapokuwa tayari kuihakikishia kampuni yake kuwa itaendelea kununua zao hilo la kahawa wilayani humo kwa kipindi kijacho tofauti na sasa ambapo kampuni yake imekuwa ikiwekewa vizingiti kadhaa vya kibiashara.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Gabriel Kimoro ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya Pembejeo ya wilaya kwa mujibu wa taratibu, alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya kiganjani ili kuelezea kwa ujumla wake juu ya suala la pembejeo wilayani humo hakuweza kupokea simu ambayo ilikuwa ikiita na kukatika.

No comments: