Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), akiwa hoi jana siku ya jumapili baada ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Iyunga(kushoto) na Mwenyekiti wa kitongoji cha Ikuti Bwana Emanuel Mwasote(katikati mwenye shati ya pink) wakijaribu kuokoa maisha ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), kwa kumpeleka Kituo cha polisi Iyunga, baada ya wananchi wenye hasira kali kuvamia kwenye nyumba yake na kutaka kuichoma moto jana siku ya jumapili kabla ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina. Hata hivyo juhudi hizo ziligonga mwamba baada ya wananchi hao kuwazidi nguvu polisi kutokana na Jeshi la polisi kushindwa kufika mapema eneo la tukio na kuaanza kumdondoshea kichapo.
Bwana Richard Mwakalinga akijaribu kuokoa maisha ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani),wakati wananchi wa kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga jijini hapa kuanza kumdondoshea kichapo jana siku ya jumapiliwakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina, wakati Jeshi la polisi halijafika eneo la tukio ili kuwedha kuwadhibiti wananchi hao.
Wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya, wakimpiga kwa mawe Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), hapo jana siku ya jumapili wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina.
Hapa ni nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, kabla ya kuvunjwa na yeye akiwa ndani ya nyumba hiyo baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na imani za kishirikina.
Wananchi wenye hasira kali wakivunja nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na Imani za kishirikina.
Wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimzingira Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, kabla ya kumdondoshea kichapo wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina.
Wananchi wenye hasira kali wakiendelea kuvunja nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, ambapo akina mama nao hawakukaa nyumba kushiriki tukio hili, baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na Imani za kishirikina.
Baada ya kupingwa Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, Jeshi la polisi lilifanikiwa kufika eneo la tukio na kumchukua mzee huyo na kumpeleka Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini Mbeya. Pichani ni baadhi ya askali na raia wema wakimuchukua mzee huyo na kumpeleka kwenye gari la polisi kabla ya kumkimbiza hospitali.
Mke wa Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, katikati akilia kwa uchungu na kupewa msaada na wanawake wenzake, baada ya mumewe kudondoshewa kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti, kata ya Iyunga jijini Mbeya jana siku ya jumapili wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina.(Picha na habari na Ezekiel Kamanga)
HITIMISHO
Maoni ya mtandao Jeshi la polisi linapaswa kufika kwa wakati muafaka mara baada ya kupewa taarifa, lakini pia elimu itolewe kwa wananchi kutojichukulia sheria mikononi kwani tuhuma na sio uthibitisho, kwani mahakama pekee ndio ina mamlaka ya kutoa hukumu.
1 comment:
Hii ni aibu kwa wananchi wa sehemu hiyo. Ningesema mengi, lakini niseme moja tu. Angalieni hao watoto wadogo wanaoshuhudia ukatili huo. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Je, watoto hao watakuwa watu wa aina gani? Taifa la kesho litakuwa taifa la hayawani.
Kuna pia upande wa kisaikolojia. Mtoto anaposhuhudia ukatili kama huu, mnajua athari zake kisaikolojia kwa huyu mtoto? Inatisha. Hilo ni suala la kukosekana kwa elimu miongoni mwa hao wananchi.
Post a Comment