Meneja wa kiwanda cha
Bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa
wa Mbeya(hawapo pichani) walipofanya ziara na kushiriki shindano la kuonja bia
hivi karibuni.
|
Meneja mawasiliano na Uhusiano wa TBL, Editha Mushi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Mbeya. |
Meneja mauzo na usambazaji nyanda za juu kusini VIvianus Rwezaura, akimkabidhi zawadi Keneth Ngelesi ambaye aliibuka mshindi wa pili
kwa kujikusanyia alama nne kwa tano.
|
Washindi wakiwa na
zawadi zao.
|
Mwakilishi wa gazeti la
Tanzania daima Mbeya, Christopher Nyenyembe akijaza fomu ya mashindano.
|
.Mtangazaji wa redio ya Mbeya fm Fredy Jackson (kushoto) akiuliza maswali kutoka kwa Saada Matiku ambaye alikuwa mshindi wa kwanza lakini bado alipata sifuri. |
Mwandishi wa habari wa
gazeti la Habari Leo, Joackim Nyambo akiwa sambamba na Mmiliki wa mtandao wa
Mbeya yetu, Joseph Mwaisango wakifuatilia kwa makini katika mashindano ya
kuonja bia.
|
Waandhishi wa Habari wa
Mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye chumba cha mashindano ya kuonja bia.
|
Meneja rasilimali watu George Albano akitoa somo kwa waandishi wa habari mkoa wa Mbeya |
Waandhishi wa habari
Mbeya wakipata maelezo mbali mbali kuhusiana na kiwanda cha bia cha TBL.
|
.Waandishi wa habari
Mbeya wakielekea kutembelea mitambo ya kuzalisha bia kiwandani hapo.
|
.Meneja wa Kiwanda
akitoa maelekezo.
|
Waandishi wa Habari
wakipata maelekezo mbali mbali juu ya uzalishaji wa bia.
|
Baadhi ya Wataalamu wa Kiwanda cha Bia cha TBL wakiendelea na majukumu yao. |
Muonekano wa Kiwanda |
Picha ya pamoja baada ya kumaliza Ziara. |
WAANDISHI wa Habari Mkoa wa Mbeya
hivi karibuni walifanya ziara ya kutembelea kiwanda cha bia TBL Mbeya ambapo
pia walipata nafasi ya kushiriki mashindano ya kuonja bia.
Katika shindano hilo, Mzoefu Saada
Matiku ambaye ni mwandishi wa Chanel Ten aliibuka kidedea kwa kupata alama tano
kwa tano ikiwa ni mara ya pili tangu apate nafasi kama hiyo kwenye mashindano
ya mwaka juzi.
washindi wengine ni Kenneth Ngelesi
wa Tanzania Daima aliyeibuka mshindi wa pili huku Merali Chawe wa Daily news
akiibuka kidedea katika nafasi ya tatu.
Mbali na mashindano hayo
Uongozi wa Kiwanda hicho umeilalamikia Serikali kwa kitendo cha kupandisha
ushuru kwenye vinywaji katika kila mwaka wa bajeti jambo linaloathiri
uzalishaji kwa makampuni binafsi.
Hayo yalibainishwa
na Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kiwanda cha Mbeya, Waziri Jemedari,
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari walipofanya ziara kiwandani hapo
Iyunga jijini Mbeya.
Jemedari alisema
uzalishaji wa bidhaa zao katika kiwanda cha Mbeya umepungua kutokana na
ongezeko la Kodi ambapo awali kabla ya kupandishiwa kwa kodi hiyo Kiwanda
kilikuwa kinafanya kazi masaa 24 kwa siku 7 lakini sasa kinafanya kazi masaa 24
kwa siku tatu.
Alisema hadi sasa
uzalishaji huo umepungua kwa asilimia 40 ambapo wakati mwingine hulazimika
kuzima na kupumzisha mitambo sababu kubwa ni kupungua kwa mauzo baada ya bei
kuongezeka.
Alisema uzalishaji
ulikuwa ni Hektolita 12000 hadi 6000 kwa siku lakini sasa hivi umeshuka hadi
Hektolita 400 hivyo kusababisha hata kutishia kupunguza watumishi.
Alisema kitendo cha
serikali kupandisha bei kwa mlaji kinaathiri pande nyingi ambapo Mlaji mwenyewe
nashindwa kumudu gharama za kununua bidhaa ili hali mzalishaji anaweza
anakazalisha kwa wingi lakini sokoni zisinunuliwe.
“Kama mnavyoona hizo
zote ni chupa tupu ambazo zimekosa vinywaji na zilipaswa kuwepo sokoni na hii
ni kutokana na kupandisha kodi kiholela, jambo ambalo hata Serikali haijatambua
kuwa na yenyewe imekosa mapato” alisema Meneja huyo huku akionesha chupa tupu za
bia.
Aliongeza kuwa serikali
ilipaswa kumpandishia kodi mzalishaji na sio mlaji wa mwisho jambo ambalo
linaathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Alisema kwa kufanya
hivyo ingekuwa rahisi kwa mzalishaji kuwa na mbinu mbadala ya kukusanya kodi
kwa ajili ya kuilipa Serikali tofauti na ilivyosasa ambapo Serikali huongeza
gharama ya kodi kwenye bidhaa inayopaswa kwenda sokoni.
Jemedari alisema katika
kunusuru kiwanda kisifungwe uongozi wa tbl umelazimika kupunguza bei ya
vinywaji tofauti na bei elekezi inayotakiwa kutokana na kiwango cha kodi ya
serikali ambapo Bia moja ilipaswa kuuzwa 2500 lakini kiwanda kimepunguza hadi
shilingi 2200.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment