Afisa Mahusiano Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya UWSA) Neema Stanton akizungumza na waandishi wa Habari
MAMLAKA ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mbeya(MBEYA UWSA)imewatahadharisha wateja wake uwepo wa matapeli wanaokusanya madeni bila idhini ya mamlaka.
Tahadhari hiyo imetolewa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Neema Stanton alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Ujenzi jijini Mbeya.
Stanton alisema wamejitokeza matapeli ambao wanapita nyumba kwa nyumba na kuwaonesha Ankara (BILL)za uongo na kuwataka wazilipie bill hizo kwa kuwatishia kuwaondolea huduma iwapo hawatalipa bili hizo hivyo wateja kwa woga hutoa pesa kwa kuhofia kukatiwa maji.
Alisema Mamlaka inatoa wito kwa wateja wake wote kuwa malipo yote ya Maji yafanyike Ofisini au katika benki za CRDB na NBC ambapo mteja atapewa stakabadhi ya Kielectroniki inayoonesha malipo hayo na jina la mteja aliyelipa.
Alisema Mamlaka inatoa tahadhari kwa wateja wake kuwa hawatakiwi kufanya malipo yoyote ya huduma ya maji nje ya ofosi za Mamlaka au Benki.
Aliongeza kuwa Matapeli hao wameshapita kwa wateja wengi wa Soweto, Forest ya Zamani na Forest Mpya ingawa idadi halisi ya fedha zilizochukuliwa kwa wateja bado hazijajulikana mara moja.
Na Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment