Meneja wa NMB Kanda Lecrisia Makiriye (Kulia) Akikabidhi Msaada wa Madawati kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa ambaye pia ni M-NEC Taifa kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
Meneja wa NMB Kanda Lecrisia Makiriye (Kulia) Akikabidhi Msaada wa Mashuka kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa ambaye pia ni M-NEC Taifa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Mary Mwanjelwa ambaye pia ni M-NEC Taifa akimshukuru Meneja wa NMB Kanda Lecrisia Makiriye baada ya kupokea misaada hiyo
***
BENKI ya Nmb Kanda ya Nyanda za
Juu Kusini imekabidhi msaada wa Madawati na mashuka vyenye thamani ya Shilingi
Milion 10 kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya(CCM) Dk. Mary Mwanjelwa.
Msaada huo ni pamoja na
madawati 83 na mashuka 250 ambavyo Mbunge huyo alikabidhiwa na Meneja wa Kanda
wa NMB katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Benki hiyo zilizopo Mbalizi
Road jijini Mbeya.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano hayo, Meneja wa NMB Kanda, Lecrisia Makiriye, alisema benki ya NMB
inatoa huduma zake katika jamii ya watu mbali mbali kwa kuwa ndiyo wadau
wanaofanya Benki hiyo kupata maendeleo.
Alisema wanajamii hao ambao
ndiyo wateja wao wanakumbana na changamoto mbali mbali ambazo zinawazunguka
hivyo kama wadau wa Serikali hawana budi kujitokeza na kutoa msaada pale
inapotokea.
Alisema katika msaada wa leo
Benki hiyo imetoa mashuka 250 kwa ajili ya Hospitalini na Madawati 83 kwa ajili
ya wanafunzi wa Shule za Msingi ndani ya Mkoa wa Mbeya ambao shule zao
zinaupungufu wa madawati.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Mbeya(CCM),Dk. Mary Mwanjelwa, alisema kama Mbunge mwanamke anaguswa
sana anapoona jamii inakumbwa na matatizo mbali mbali.
Alisema kutokana na jamii
kuhitaji mahitaji makubwa akaona ni vema akaomba msaada kwa Benki ya NMB kwa
ajili ya kusaidia wenye shida ambapo Benki hiyo imesikia kilio chake na kutoa
msaada huo kutokana na alivyoomba.
Alisema sehemu ya mashuka hayo
Mashuka 100 atapeleka kwa waliokumbwa na mafuriko hivi karibuni wilayani Kyela
na mashuka mengine 150 atapeleka kwa wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Mbeya.
Alisema Madawati atayagawa
katika Shule za Msingi zenye upungufu ndani ya Mkoa wa Mbeya kadri
itakavyowezekana kutokana na mahitaji ya madawati kuwa bado makubwa katika
kuinua kiwango cha Elimu mkoani Mbeya.
Aidha alitoa wito kwa taasisi
na watu binafsi kuendelea kujitolea kwa msaada wa hali na mali kwa wananchi wa
Wilaya ya Kyela kutokana na mafuriko yaliyowakuta kwamba bado hali zao
hazijatengemaa hivyo jitihada zaidi zinahitajika.
Alisema katika kuonesha
wananchi wa Kyela wanahitaji bado misaada pia Wabunge wa Mkoa wa Mbeya
wanajipanga kuhakikisha wanatoa chochote kwa ajili ya kuwasaidia wananchi
waliokumbwa na mafuriko.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment