Viongozi wa ukawa wakiongea na waandishi wa Habari
Muungano wa Katiba ya wananchi
(UKAWA) wanatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara kesho kwenye viwanja vya
shule ya msingi RuandaNzovwe jijini Mbeya.
Mkutano huo utahutubiwa na Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi(CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba,pamoja na viongozi wengine
akiwepo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(SUGU)
Ukawa inaundwa na muungano wa
vyama vitatu vya siasa ambavyo ni Chadema, Cuf pamoja na NCCR-Mageuzi ambao
wamekuwa wakizunguka sehemu mbali mbali kuzungumzia katiba mpya na serikali
tatu.
Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija,katika
mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya
Mbeya Peak, asema taratibu zote za mkutano huo zimekamilika.
Mwambigija amesema mbali na
taratibu zote kukamilika lakini maandalizi yake yamekumbana na vikwazo vingi
ikiwemo Jeshi la Polisi kukatalia kibali cha kufanya maandamano wakati wa
mapokezi ya Mwenyekiti wa CUF Taifa Profesa Lipumba.
Amesema mbali na kukataliwa
kibali cha maandamano pia Halmashauri ya Jiji la Mbeya pia limekataa kupokea
malipo kwa ajili ya gari la Matangazo(PA) jambo alilodai ni kuwanyima haki ya
kikatiba ya kufanya maandamano pamoja na watendaji wa Serikali kuingiliwa na
wanasiasa.
Amesema pamoja na changamoto
hizo Mkutano utafanyika kama ilivyopangwa isipokuwa maandamano hayatakuwepo
pamoja na wafuasi wao hawataruhusiwa kushika mabango ya aina yoyote ili kuepuka
kuhujumiwa na upinzani wao ambao ni Chama cha Mapinduzi.
Ameongeza kuwa kukiwa na
mabango CCM hupenyeza watu wake ambao hushika mabango ya kukashifu UKAWA pamoja
na kupinga suala la serikali tatu katika mikutano yao kwa kuwavalisha sare za
Chadema na UKAWA.
Amesema hali kama hizo
zimeshajitokeza katika mikutano iliyofanyika Iringa na maeneo mengine ambapo
baada ya kufanya uchunguzi wanabaini kuwa siyo wanachama wao bali ni mamluki
waliopandikizwa kwa lengo la kutoa ujumbe tofauti na malengo.
Mwambigija amesema mtu yoyote
atakayeonekana na bango la aina yoyote atapata cha moto kutoka kwa vijana wa
Red briged ambao watakuwa wakilinda eneo la mkutano pamoja na kufanya doria
usiku kucha kuangalia kama kuna dalili zozote za kuandaa mabango.
No comments:
Post a Comment