SIKU chache baada ya wakazi wa Jiji la Mbeya kupewa tahadhari juu ya uwepo wa nyoka mkubwa aina ya Chatu katika maeneo ya Rift Valley pembezoni mwa mto Meta uliopo jijini hapa juhudi za kumsaka zaanza kuzaa matunda.
Juhudi za kumsaka Chatu huyo zilianza juzi kwa ushirikiano wa Wataalamu wa Wanyamapori pamoja na waganga wa jadi ambao walikuwa wakimsaka pembezoni mwa mtu huo.
Hata hivyo jitihada za klumsaka Nyoka huyo zilianza kuzaa matunda baada ya jana asubuhi Waganga hao kufanikiwa kumnasa Chatu mdogo pembezoni mwa Mto Meta karibu na Hoteli ya Rift Valley.
Kwa mujibu wa Mganga huyo, Mazoea Hamis(39) mkazi wa Chalinze mkoani Pwani alisema siku ya kwanza ya zoezi hilo walifanikiwa kugundua njia alimokuwa amepita lakini hawakufanikiwa kumpata.
Alisema jioni yake baada ya kupumzika waliona waweke dawa za kienyeji ambazo zingiweza kumtoa mafichoni na kusogea karibu ambapo asubuhi waliwahi kuendelea kumtafuta.
Alisema baada ya muda kidogo wakati akiendelea kufyeka vichaka lakini kwa bahati nzuri alimkanyaga chatu huyo na yeye kukurupuka ndipo alipofanikiwa kumkamata.
Kwa mujibu wa mganga huyo ambaye anasaidiwa na Athman Keneth(30) mkazi wa Chunya mkoani hapa, alisema Chatu huyo ni mdogo na juhudi za kuendelea kumtafuta mkubwa zitaendelea kama kweli yupo.
Alisema mara nyingi Chatu mdogo anapoonekana Mkubwa anakuwa amehama ili kuwapisha wadogo kuendelea na maisha yao ama huyo mdogo alisombwa na maji kipindi cha mvua kutoka kwenye hifadhi na wenzie.
Hata hivyo taarifa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji zinadai kuwa baada ya kukamatwa kwa Chatu huyo atahifadhiwa na kutunzwa katika Hifadhi ya Wanyama ya Ifisi ambako kuna wanyamapori wengine wa maonesho.
NA MBEYA YETU
No comments:
Post a Comment