Jamaa hana hata wasisi juu ya mtoto wake yee anasema ni mipango ya mungu tu
Mtoto jinsi
ya kiume aliyefahamika kwa jina la Suleiman Kolineli(miezi kumi) mkazi wa
kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya aliyezaliwa na
ulemavu wa mdomo(mdomo sungura)amefikishwa Hospitali ya Rufaa Mbeya ili
kupatiwa matibabu.
Mtoto huyo
ambaye alifichwa na wazazi wake baada ya kuzaliwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Chunya na kutakiwa kurudi Hospitali hiyo baada ya miezi sita ili afanyiwe
upasuaji kurekebisha sura yake lakini wazazi wake walishindwa kumpeleka
Hospitali wakidai huo ni mpango wa Mungu.
Baba mzazi
wa mtoto huyo Kolineli Mushi(34) amesema hakuwa tayari kumpeleka Hospitali kwa
kuwa ulemavu huo umetokana na Mungu na kwamba akitibiwa nyumbani kwao watapata
matatizo au kutokea kitu ingawa hakuwa tayari kubainisha matatizo hayo.
Kwa upande
wake mama mzazi wa mtoto Yohana Kolineli(37)amesema licha ya kutakiwa kumpeleka
mtoto Hospitali ya Wilaya ya Chunya alikosa nguvu kutokana na mume wake kukataa
kata kata kushughulikia suala hilo kwa kisingizio cha kuwa ni mpango wa Mungu.
Kwa upande
wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya Frank Ngalla amekiri kuzaliwa
na tatizo kwa mtoto huyo na kawaida watoto wadogo huanza kufanyiwa upasuaji
miezi sia baada ya kuzaliwa na mtoto awe na uzito usiopungua kilo 5 hivyo
walimtaka mzazi kurudi na mtoto kwa kipindi cha muda huo lakini hawakutokea
Hospitali.
Mtoto huyo
ambaye hula na kupumua kwa shida hivi sasa ana uzito wa kilo8.6 anahitaji
msaada wa upasuaji haraka ili kumfanya ale vizuri na kupumua vizuri kwani mama
mzazi hupata shida wakati wa kulsha na chakula kuwa hatarini kuingia kati koo
la hewa kutokana na uwazi kati ya pua na mdomo.
Afisa Ustawi
wa jamii Hospitali ya Rufaa Mbeya Anna Geleta amesema matibabu ya ugonjwa huo
ni bure na wakati mwingine hufanywa na Madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa
Mbeya au Hospitali ya CCBRT ya Dar es Salaam na kubainisha kuwa maandalizi
yamefanyika ili mtoto huyo asafirishwe kwenda kutibiwa CCBRT.
Mtoto huyo
amegunduliwa na waandishi wa Habari wa Mbeya yetu waliokuwa wametembelea Kijiji
cha Igundu ambapo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Emmanuel Mbughi aliridhia mtoto kupatiwa
matibabu na kwamba mtoto mwenye ulemavu kama huo hayupo na hakupata taarifa za
ulemavu huo.
Katibu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Aisha Mtanda amesema taratibu za kumsafirisha mtoto na
mama yake zimekamilika na kutoa wito kwa wazazi na walezi kutowafungia ndani
watoto wenye ulemavu wowote,aidha amewataka pia wanawake wanaosumbumbuliwa na
ugonjwa wa Fistula wajitokeze katika Hospitali Rufaa ili kutibiwa bure.
Mtanda
amesema Madaktari bingwa nchini wataanza kuwahudumia wagonjwa wa Fistula kutoka
mikoa ya nyanda za juu kusini kuanzia Mei 12 hadi Mei 23 mwaka huu bila gharama
zozote hivyo wagonjwa wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwani Fistula inatibika.
Na Mbeya yetu
|
1 comment:
Kweli inasikitisha sana
Post a Comment