Add caption
LIGI ya Mpira wa miguu ya Kombe la
Mastala linatarajia kuanza kutimua vumbi Mei 10, Mwaka huu katika viwanja vya
Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi
wa Habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mtenda ilioyopo Soweto jijini
hapa, Mratibu wa Ligi hiyo, Willy Mastala alisema jumla ya timu 20
zimethibitisha kushiriki ligi hiyo.
Mastala aliongeza kuwa ligi hiyo
imedhaminiwa na Kampuni ya Soda ya Cocacola Kwanza Mbeya kwa udhamini wa
shilingi Milioni Tano zitakazotumika kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa
tatu.
Alizitaja zawadi hizo kuwa ni pamoja na
mshindi wa kwanza atakaeibuka na kitita cha shilingi Milioni 2, Mshindi wa pili
shilingi milioni 1 na mshindi wa tatu akiibuka na shilingi Laki 5 ambapo zawadi
ya mfungaji bora ikiwa ni shilingi Laki moja inayotolewa na Bomba fm redio.
Alisema timu hizo zitacheza kwa mtindo
wa ligi ambapo timu zitagawanywa kwenye makundi manne yenye timu tano kila
kundi na kisha kupata timu mbili zitakazoingia katika hatua za Nusu fainali,
robo na hatimaye fainali.
Alisema kabla ya kuanza kutimua vumbi
katika ligi hiyo itatanguliwa na mtanange mkali wa ngao ya Hisani kati ya timu
ya Zaragoza fc na Ilemi ambazo zilikuwa kwenye nafasi za juu msimu uliopita.
Alizitaja timu hizo kuwa kundi
A,Vijana,Sido Junior,Kabwe United, Pamba nyepesi na FC Leopard, kundi B
linaundwa na timu za Cocacola, Airport Rangers, Majiko fc, Sidon a Ilemi, Kundi
C lina timu za Wakongwe, Terminal, Wateule, Moning Star na Zaragoza huku kundi
la Nne likiwa na timu za Mbaspo, Two in One, Kibogozo, Felali na Chuma chakavu.
Kwa upande wake Meneja usambazaji wa
Kampuni ya Cocacola kanda ya Nyanda za juu kusini, Emmanuel Mnyoga, alisema
wanajisikia fahari kusaidia kuinua vipaji vya michezo kuanzia ngazi za chini
kupitia udhamini wanaoutoa.
Alisema kutoa udhamini kwenye michezo ni
sehemu moja wapo ya kurudisha fadhila kwa wateja wao na kutoa mchango katika
jamii inayoizunguka kutokana na vipaji vianavyoibuliwa hutokea katika familia
za kawaida.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment