Wananchi wakifuatilia kikao cha baraza la madiwani Wilaya ya Mbarali.
Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Modest Kilufi akichangia jambo kwenye mkutano wa Baraza.
Baraza la Madiwani la Wilaya ya Mbarali likiendelea na kikao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Kenneth Ndingo akiongoza kikao cha baraza la madiwani.
**************************
HATIMAYE Baraza la Madiwani Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya
limefuta ushuru wa mazao wa shilingi elfu mbili kwa gunia uliokuwa ukitozwa kwa
wakulima Wilayani humo ili kuepusha mgogoro ulokuwepo.
Kufutwa kwa ushuru huo kumekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Abbas Kandoro kupokea malalamiko kutoka kwa Wakulima wa Wilaya ya Mbarali ambao
walidai kutozwa ushurukwenye mpunga ambao umevunwa kwa ajili ya chakula na siyo
biashara.
Mkuu wa Mkoa aliagiza kuitishwa kwa Baraza la dharula ili kujadili
mustakabali wa suala hilo, ambapo Baraza lilitii agizo na kufanya kikao Mei 27,mwaka huu katika ukumbi wa Maji Mbarali
na kuamua kutengua ushuru huo uliokuwa umepitishwa na Madiwani hao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Keneth Ndingo,
katika hotuba yake alisema Halmashauri inatakiwa kufikiria vyanzo vingine ili
kuziba pengo hilo ambalo ni hasara ya
zaidi ya shilingi milioni 640.
Alisema Baraza limeridhia
kupunguza mawakala wa kukusanya ushuru kutoka kumi wa awali na kubakia wanne
ili kuleta ufanisi wa mapato na kurahisisha udhibiti wa mapato ili kuondokana
na hati chafu ya ukaguzi.
Alisema katika mpango mpya kutakuwa na kanda mbili za makusanyo
ambazo ni kutoka Tarafa ya Rujewa na Tarafa ya Ilongo na kila Tarafa kutoa
mawakala wawili watakaokusanya ushuru kwa ufanisi na kuboresha mapato ya
Halmashauri.
Mmoja wa wakulima Christopher Uhagile aliyehudhuria kikao hicho
maalumu alimpongeza mkuu wa Mkoa Abbas Kandoro kwa kuchukua hatua za haraka
kuitisha Baraza hilo kwani amani ilitoweka kutokana na mkanganyiko uliojitokeza
baada ya kuanza utekelezwaji wa sheria ya ukusanywaji wa ushuru kwa mkulima.
Baadhi ya Madiwani walimlalamikia Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Modestus
Kilufi, kuwa kitendo cha kuhoji ushuru uliopitishwa na baraza ni usaliti.
Walisema mkulima kutozwa
ushuru wakati yeye ni mjumbe wa Baraza na alikuwa miongoni mwa wajumbe
waliopitisha mkulima kutozwa ushuru wa mazao hivyo hakupaswa kuhoji chochote
kwani kauli hiyo ni ya kuwachonganisha wakulima.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gullam Hussein Kiffu
aliwataka watendaji wote wa Halmashauri na Madiwani kushirikiana ili kukusanya
mapato yatakayowezesha Halmashauri kujiendesha na kuleta maendeleo kwa
wananchi.
NA MBEYA YETU
No comments:
Post a Comment