Venance Matinya kutoka mtandao wa Mbeya yetu Blog akipokea Hati ya shukrani kutoka kwa Mgeni Rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya, Thobias Mwalwego kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa kwa kutambua mchango wa Mbeya yetu Blog katika kulea watoto yatima
mwanafunzi aliyehitimu fani ya ufundi wa magari akikabidhiwa vifaa vyake.
Mwanafunzi aliyehitimu fani ya kilimo cha mbaogamboga akikabidhiwa vitendea kazi.
Mwanafunzi wa fani ya useremala naye akikabidhiwa vitendea kazi.
Mgeni rasmi, Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Mbeya, Thobias Mwalwego
akihutubia katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro.
Mwanafunzi wa fani ya ushonaji akikabidhiwa vitendea kazi ambacho ni Cherehani.
Meneja wa Kituo, Amanda Fihavango akiwaeleza jambo waandishi wa habari
.Mkurugenzi wa Nuru Orphans centre Jasson Fihavango akisoma risala.
Mwanafunzi akikabidhiwa cheti cha kuhitimu masomo
yake.
Wageni waalikwa wakitembelea majengo ya kituo cha nuru.
KITUO cha Nuru Ophans kimekabidhi
vitendea kazi kwa vijana wanaoishi kwenye mazingira magumu Mbeya baada ya
kuhitimu mafunzo ya fani mbali mbali kutoka Chuo cha ufundi Veta mkoani Mbeya.
Hafla hiyo ilifanyika juzi
katika makao makuu ya kituo hicho kilichopo Uyole Jijini Mbeya ambapo vijana 30
walipewa vyeti vya kuhitimu masomo yao pamoja na vifaa vya kufanyia kazi.
Meneja Miradi wa Nuru Ophans Centre,
Osward Poyo,alisema Asasi yake baada ya kufanya utafiti ilibaini kuwepo kwa
vijana wanaoishi katika mazingira magumu
2500 katika kata 6.
Alisema baada ya kubaini hayo
Asasi hiyo iliomba msaada kwa Ubalozi wa Marekani nchini kwa ajili ya
kuwasomesha vijana hao fani mbali mbali za ufundi lakini Ubalozi ulikubali
kuwasomesha vijana 30 tu hivyo kufanya kila kata kutoa vijana 5.
Aliongeza kuwa Ubalozi wa
Marekani baada ya kutiliana sahihi mkataba wa kuwasomesha vijana hao walitoa
jumla ya shilingi 16,800,000 kwa malipo ya ada, Nauli ya kwenda na kurudi
chuoni, malipo ya chakula kwa siku zote za masomo na ununuzi wa Vitendea kazi
kulingana na fani ambazo vijana wamesomea.
Alizitaja fani ambazo vijana
hao wamesomea na vifaa walivyokabidhiwa kuwa ni pamoja na fani ya Ushonaji
ambayo ilikuwa na vijana 12 waliokabidhiwa Cherehani kila mmoja,Seremala kijana
mmoja aliyekabidhiwa Misumeno 3,Landa 2, Nyundo pamoja na Ovaroli.
Wengine ni fani za Ufundi
magari ambao ulikuwa na vijana 6 ambao kila mmoja alikabidhiwa Ovaroli,dazani
ya spana na Jeki ya kuinulia magari na vijana 9 waliochukua fani ya udereva
ambao walipewa Leseni za kuendeshea magari na vijana wawili waliosoma fani ya
klilimo cha mboga mboga ambao walipewa kila mmoja kilo 50 za mbolea aina ya
Urea, Mbegu za mahindi kilo 6, Pumpu ya kunyunyizia dawa 1 pamoja na mbegu za
mboga za nyanya, spinachi na karoti.
Naye Mgeni rasmi katika hafla
hiyo, Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Mbeya,Thobias Mwalwego, ambaye
alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alitoa wito kwa vijana wa
fani za ufundi kuwa waaminifu kwa wateja wao na huduma watakazokuwa wakitoa kwa
manufaa ya jamii nzima.
Alisema vifaa walivyokabidhiwa
vinafaa kutunzwa na siyo kukimbilia kuuza hali ambayo inaweza kuwarudisha
katika hali ya awali ya kuzurura mitaani bila kuwa na fani ya kufanya.
Na Mbeya yetu Blog
No comments:
Post a Comment