Baadhi ya wananchi wakiwa wanaendelea kutoa takataka nje ya Ghuba na kuziweka katika sehemu husika ukiwemo na Mzoga wa Mbwa .
MKURUGENZI
wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Mussa Zungiza, amesema tatizo la uchafu uliopo
katika maeneo mbalimbali Jijini umetokana na kuharibika kwa maghuba kumi ya
kuzolea taka.
Zungiza alisema chanzo cha kuharibika kwa maghuba hayo kumetokana
na watumiaji wa maghuba hayo kuchoma taka ndani ya maghuba hayo ali
inayopelekea kupasuka na kuvujisha taka.
Alisema
kutokana na kuharibika kwa maghuba hayo maeneo mbalimbali yameathirika na
kusababisha wananchi kutupa taka chini na kwamba magari yaliyopo kwa ajili ya
kuzoa taka ni machache hivyo kuleta mrundikano wa taka kwa muda mrefu na kuwa
kero kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kutupa
taka.
Mkurugenzi alisema tangu amefika Jijini Mbeya ameweza kukarabati
maghuba sita yaliyokuwa yameharibika na sasa maghuba kumi yameharibika hivyo
wako mbioni kukatabati pindi utaratibu wa serikali katika manunuzi kukamilika.
Alisema kutokana na
uzalishaji mkubwa wa taka unaotokana na ungezeko la wakazi na viwanda wameagiza
maghuba mengine 84 yatkayoondoa kero ya muda mrefu ya mrundikano wa taka Jijini
Mbeya.
Aidha alisema hivi sasa wanajitahidi kuzoa kwa kutumia magari
yaliyopo ingawa yanalemewa na uwingi wa taka katika Kata 36 za Jiji ni magari
matatu tu yanayofanya kazi kila siku hivyo baadhi ya maeneo ya masoko
kutopitiwa mara kwa mara na magari hayo.
Aliongeza pia mkakati wa Serikali ni kuongeza magari mengine ya
kuzolea taka sambamba na marekebisho ya magari ya kisasa ya kuzolea taka ambapo
mazungumzo ya awali baina ya Jiji na Wahisani kutoka China yanaendelea vizuri.
Kwa upande wake Afisa Usafishaji Jiji la Mbeya Samwel Bubegwa alisema
kuwa mbali ya mikakati hiyo Halmashauri ya Jiji inakusudia kubinafsisha
shughuli za usafi kwa vikundi vya vijana vitakavyokuwa na jukumu la usafi
katika kila Kata hivyo kuongeza ajira kwa vijana katika kila Kata.
Bubegwa alisema utafiti uliofanywa katika Kata ya Iyunga umeonesha
mafanikio makubwa hivyo mbali ya kutoa ajira utaboresha usafi katika maeneo
yote kutokana na vikundi hivyo kuwa karibu ya wananchi.
Afisa huyo alisema hivi sasa vijana katika kila Kata wajiunge ili
kuanzisha vikundi hivyo kwani Jiji litatoa tenda kwa vikundi na si mtu binafsi
ili vijana waondokane na tatizo la ukosefu wa ajira.
Mkurugenzi Mussa Zungiza amemaliza kwa kutoa wito kwa wananchi
kushirikiana na Jiji la Mbeya kwa kufuata taratibu za usafi ikiwa ni pamoja na
kuacha kutupa samadi katika maghuba na mizoga hali inayohatarisha afya za
wakazi wanaoishi karibu na maghuba kuwa hatarini na magonjwa yanayotokana na
hewa.
NA MBEYA YETU
No comments:
Post a Comment