MWANAFUNZI
Marha Jackson(13) wa darasa la sita Shule ya Msingi Mwasote iliyopo Kata ya
Nsalaga Uyole Jijini Mbeya, ambaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha
nyumbani kwao Disemba 17, 2013 amepatikana eneo la Tunduma akitokea Ilula
Mkoani Iringa.
Baadhi
ya mashuhuda waliomuona binti huyo walipomuuliza mahala alipokuwa akiishi na
mazingira aliyoondokea nyumbani kwao alisema alichukuliwa na bibi yake
aliyemtaja kwa jina la Hidaya Yailah Mussa(35)anayemiliki mgahawa eneo la Mtuha
uliopo Ilula Mkoani Iringa ambako alidai alikuwa akitumikishwa na bibi yake
huyo katika shughuli mbali mbali akiwa na wenzake kumi.
Alisema
alichukuliwa na bibi yake huyo kutoka Nsalaga hadi Mlima Nyoka ambapo baada ya
kufika huko walipanda kitu kilichodaiwa ni ndege hadi Ilula ambako walipelekwa
moja kwa moja kufanya kazi katika mashamba ya Nyanya, Pilipili na Mahindi huku
wao wakiwa wakilishwaMananasi na mahindi.
Mwanafunzi
huyo alisema siku ya kwanza walifikia makaburini ambako aliwakuta watu wengi
ambapo aliweza kuwatambua baadhi yaokwa majina ambapo waliendelea na kazi za
bibi huyo hadi siku ambayo aliamua kuondoka na kujikuta akiwa amesimama katika
eneo la Sogea Tunduma wilaya ya Momba Mkoani hapa.
Aliongeza
kuwa hadi kufika eneo hilo alitumia usafiri ule ule unaodaiwa kuwa ni ndege na
baada ya kutua alikutana na mama yake mzazi aliyemtaja kwa jina la Agnetha
Joseph(37) Mkazi wa Sogea Mji mdogo wa Tunduma ambaye hakumtambua mara moja
kutokana na kutokuwa na ufahamu kwa wakati huo na kumuona kama watu wengine wa
kawaida.
Alisema
wakiwa shambani walifanyishwa kazi bila malipo yoyote na kuambulia kulishwa
mahindi na mananasi huku Nyama wakilishwa mara chache baada ya kuletewa na bibi
yake huyo.
kwa
upande wake mama mzazi wa binti huyo Agnetha Joseph alisema alipatwa na mshtuko
kuona mwanae akiingia nyumbani huku akiwa amechafuka sana majira ya saa tatu
usiku huku akiwa hana fahamu sawa sawa hali iliyomlazimu kumpeleka Nsalaga
alikokuwa akiishi awali na bibi yake.
Kupatikana
kwa mtoto huyo kumetokana na juhudi zilizofanywa na Muungano wa Jamii
Tanzania(MUJATA) ambao mara nyingi wamekuwa wakikemea vikali vitendo
vinavyotokana na imani za kishirikina ndani na nje ya Mkoa wa Mbeya.
Mwenyekiti
wa Mujata, Chifu Shayo Soja Masoko alisema kupatikana kwa mtoto huyo akiwa ni
mzima ni kutokana na taarifa walizozipata kutoka kwa wataalamu wa jadi
waliobainishwa uwepo wa mtoto akiwa hai na kuchukuliwa kwa imani za
kishirikina.
Alisema
baada ya kufanya vitu vyao waliweka mtego wa kumbaini mtu anayehusika na
vitendo hivyo jambo ambalo lilizaa matunda kwa kujitokeza mbele yao Mwanamke
mmoja aliyefahamika kwa jina la Hidaya Mussa ambaye aliwasili Mbeya Machi 15
akiwa ameambatana na baba mzazi wa binti huyo aliyejulikana kwa jina la Kulwa
Khatibu.
Mzazi
wa Binti huyo Kulwa Khatibu ambaye ni mkazi wa Tabata Jijini Dar Es Salaam
alisema hakuwa na taarifa za kupotea kwa mtoto wake kutokana na yeye muda
mwingi kuwa kikazi Mkoani Mtwara hivyo kukosa imani na taarifa za kupotea kwa
mwanae huyo hadi aliposikia ameonekana jambo lililomlazimu kufika kujionea hali
halisi.
Kwa
upande wake Chifu Soja alipomhoji Hidaya kuhusiana na upotevu wa Mwanafunzi
huyo alikiri kumuona Ilula na kuongeza kuwa kuna mzee mmoja kijijini kwao
ambaye anahusishwa na matukio ya kuwachukua misukule watoto wa watu na kuahidi
kutoa ushirikiano kwa Mujata ili kumbaini mzee huyo jambo ambalo halikueleweka
vizuri kwa wananchi waliokuwa wamefurika hadi na kuzua taflani iliyolazimu
Jeshi la Polisi kumchukua na kuondoka naye.
Mwisho.
NaEzekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment