Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, March 19, 2014

AIR TANZANIA YAANZA SAFAZI ZAKE MBEYA




Mkurugenzi Msaidizi wa Biashara Juma Boma ambaye amesema kwa kuanzia shirika lake litafanya safari nne kwa juma kwa gharama ya shilingi laki moja na elfu hamsini tu kwa safari moja ya kwenda.

Marubani wa Ndege hiyo

 Patrick Itula ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa Ufundi wa shirika hilo amesema hivi sasa Mkoa wa Mbeya unazo fursa za kukuza biashara kupitia shirika lake kutokana kuwa na mpango wa kuunganisha safari zake kutoka Mbeya na kwenda mikoa ya kaskazini na kanada ya ziwa.






Rubani wa ndege hiyo Richard Shaidi ameipongeza serikali kwa kukamilisha uwanja huo kwani ni mzuri na umekuwa miongoni mwa viwanja bora nchini na unaweza kutua wakati wowote kutokana na kufungwa vifaa vya kisasa.





Shirika la ndege nchini[ATC]limeanza safari za anga kutoka Dar es Salaam na Mbeya Machi 17 mwaka huu.

Safari ya kwanza ya ndege hiyo imezinduliwa rasmi na Mkurugenzi Msaidizi wa Biashara Juma Boma ambaye amesema kwa kuanzia shirika lake litafanya safari nne kwa juma kwa gharama ya shilingi laki moja na elfu hamsini tu kwa safari moja ya kwenda.

wanazo ndege bora ambazo wasafiri watafurahia huduma zake wawapo safarini, Boma amesema shirika lake limejipanga vema kukabiliana na ushindani uliopo .

Pia amesema kuwa shirika lake limezingatia matakwa ya wateja hivyo ndege zake zitaanza safari Dar es Salaam saa sita mchana na kufika Mbeya saa saba mchana ili kuwawezesha abiria wanaotoka nchi jirani kusini mwa Afrika kuwahi safari ili kutumia ndege za ATC.

Aidha Patrick Itula ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa Ufundi wa shirika hilo amesema hivi sasa Mkoa wa Mbeya unazo fursa za kukuza biashara kupitia shirika lake kutokana kuwa na mpango wa kuunganisha safari zake kutoka Mbeya na kwenda mikoa ya kaskazini na kanada ya ziwa.

Itula amesema kuwa pia wana mpango wa kuanzisha safari za kwenda Congo na Zambia kupitia Mbeya ili kuimarisha zaidi biashara ya utalii kwani Mkoa wa Mbeya una vivutio vingi hivyo Mkoa utatumia fursa kujitangaza.

Kwa upande wake Rubani wa ndege hiyo Richard Shaidi ameipongeza serikali kwa kukamilisha uwanja huo kwani ni mzuri na umekuwa miongoni mwa viwanja bora nchini na unaweza kutua wakati wowote kutokana na kufungwa vifaa vya kisasa.

Na Mbeya yetu

No comments: