Add caption
Wananchi wa Mji mdogo wa Mbalizi Wilaya
ya Mbeya nje kidogo ya Jiji la Mbeya walijikuta katika wakati mgumu baada ya
kupata matukio mawili makubwa kwa wakati mmoja huku watu kadhaa wakihofiwa
kujeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali Teule ya Ifisi kwa ajili ya Matibabu.
Tukio la kwanza kuwakumba wakazi hao ni
kumbunga kilichoambatana na upepo mkali ambacho kiliezua nyumba zaidi ya 30
yakiwemo Makanisa na kujeruhi watu ambao idadi yao haijafahamika maramoja
ambao walikimbizwa Hospitali na kutibiwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo
walisema Kimbunga hicho kilianza majira ya saa Sita Mchana leo
kikivikumba vitongoji vya Iwindi, Jeshini, Mtakuja na Tarafani ambapo kimbunga
hicho kiliezua mapaa ya nyumba za kuishi, maduka pamoja na makanisa.
Hata hivyo tathimini ya hasara
iliyotokea bado haijajulikana ikiwa ni pamoja na idadi ya majeruhi na hali yao
kutokana na wasemaji wa matukio hayo kutopatikana kwa wakati.
Hata hivyo katika tukio lingine
lililotokea katika Stendi ya zamani Mbalizi ambapo kwa sasa ni kituo cha magari
madogo yanayosubiri kukodiwa, walijikuta katika wakati mgumu baada ya kutokea
kwa ajali mbaya iliyohusisha magari 9 na kujeruhi watu waliokuwemo.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo
cha ajali hiyo iliyotokea majira ya Saa Nane mchana ni gari aina ya Canter
yenye namba za usajili T 186 AMM ambalo lilikatisha barabara bila kuangalia
tahadhali likiwa linatokea barabara ya Utengule na kuvuka barabara ya TanZam
likielekea barabara ya Kituo cha Polisi.
Walisema baada ya gari hiyo kuingia
barabarani ilikutana na Roli kubwa lenye namba za usajili T 731 BLM likiwa na
Trela lenye namba T 126 BKS ambalo katika harakati ya kulikwepa
lilipoteza mwelekeo na kuyagonga magari mengine ambayo yalikuwa yameegeshwa.
Magari yaliyokumbwa na adha hiyo ni
pamoja na Fuso aina ya Tipa lenye namba za usajili T 402 CEP, Toyota Pick up
yenye namba T 367 ADR, Toyota Corola T 330 BRL, Nissan Pick up T 651 ACG,
Sprinter T 860AXL, Ipsum T640 CDE na Nadia T 509 BGZ.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment