Maandalizi
ya Ligi ya mpira wa miguu kwa madereva wa bodaboda yameshika kasi ambapo
waandaaji wa ligi hiyo wameanza kutekeleza ahadi yao kwa kuwaunganisha na
mifuko ya jamii.
Msemaji
wa mfuko wa jamii wa PPF amewataka Madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la
Bodaboda kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kulingana na vipato vyao
kwa manufaa ya maisha ya baadaye.
Mwito
huo ulitolewa na mwakilishi wa Mfuko wa jamii wa PPF kanda ya Mbeya, Nyemo
Chomola, alipokuwa akizungumza na viongozi wa vituo vya boda boda Jiji la Mbeya
alipokuwa akiwahamasisha na kujiunga na mfuko huo katika mkutano ulioitishwa na
Kampuni ya Citysign Promotion & Markerting Agency Limited ya Jijini Mbeya
kwa ajili ya maandalizi ya ligi ya mpira wa miguu( Boda boda cup 2014).
Nyemo
alisema vijana wa boda boda wanaweza kunufaika na mfuko huo kwaajili ya maisha
yao kutokana na mfuko huo kumlenga mjasiliamali yoyote kuhifadhi akiba zake
kulingana na kipato chake.
Alisema
mfuko wa Hifadhi ya jamii wa PPF unawasaidia wanachama wake kutunza akiba zao
kwa maisha ya baadaye ambapo mwanachama anauwezo wa kunufaika na mafao saba
ambayo ni mafao ya uzeeni, kifo,ugonjwa, wategemezi, kujitoa,elimu na kiinua
mgongo.
Alisema
mafao hayo ni muhimu sana kwa madereva wa boda boda kwa kuwa wengi ni vijana na
kazi wanayofanya ni hatari kutokana na kupata ajali nyingi za mara kwa mara
hivyo kupitia mfuko huo unaweza kuwasaidia baada ya kupata matatizo kwa
kunufaisha mwenyewe au wategemezi.
Awali
wakijadili mfumo wa ligi hiyo mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Geophrey
Mwangunguru katika kikao cha maandalizi baina yao na viongozi wa chama cha
waendesha bodaboda kilichofanyika katika viwanja vya City pub Jijini Mbeya
alisema ligi hiyo itakuwa na timu 16 ambazo zitatoka katika kanda sita za
bodaboda jijini Mbeya.
Alizitaja
kanda hizo kuwa ni Kanda ya Sae, Kabwe, Iyunga na Uyole ambazo zitatoa timu 3
kila mmoja huku kanda ya Mafiati na Kadeghe zikitoa timo moja moja.
Mwaangungulu
alisema lengo la kuandaa ligi hiyo ni kuwaunganisha madereva wa bodaboda ili
kusudi waweze kutambuliwa na wanajamii ambao asilimia kubwa wamekuwa
wakiwatuhumu kwamba ni wakorofi waliokosa ustarabu na umoja.
Alisema
kupitia ligi hiyo wataweza kupata faida kubwa kwa kupatiwa elimu mbalimbali zikiwemo
usalama barabarani ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima,kuunganishwa na
mifuko ya jamii, bima za afya,saccos na jinsi ya kujiwekea akiba.
Aliongeza
kuwa ligi hiyo intarajiwa kuanza kulindima mapema mwezi wa nne baada taratibu
zote kukamilika kwa kuzihusisha timu zaidi ya 16 za vituo vya bodaboda.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa shirikisho la mpira wa miguu Jiji
la Mbeya(MUFA) Ramadhani Lulandala alisema ni vema madereva wa bodaboda
wakajiandaa vizuri huku wakitambua sheria na kanuni za mpira wa miguu kwa
kuepuka kuwafanyia vurugu waamuzi na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua
kali za kisheria.
Aidha
kwa upande wao viongozi wa boda boda wakiongozwa na Mwenyekiti wao Vicent
Mwashoma na katibu Msumba Mdesa waliwapongeza waandaaji wa ligi hiyo kwa
kuwakumbuka waendesha bodaboda na kuwahakikishia kushiriki ligi hiyo kwa amani
na kwamba haina haja ya kulihusisha jeshi la polisi kwa madai kuwa wanauwezo wa
kudhibitina wao wenyewe.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment