Maombi ya kuahirishwa kwa kesi hiyo yalitolewa na Mwendesha mashtaka wa Serikali, Basilius Namkambe ambapo aliiambia Mahakama mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Michael Mateite kuwa Mahakama haiwezi kuendelea na kesi kutokana na hali ya Mshtakiwa.
Alisema upande wa Mashtaka, Mahakama na upande wa utetezi wote umejiridhisha na hali ya Mshtakiwa namba mbili, Elinanzi Mshana(22)Mkazi wa Iyela Jijini Mbeya kuwa na jeraha litakalomfanya kushindwa kusikiliza kesi yake.
Aliiomba Mahakama kupanga siku nyingine ya kusikiliza kesi hiyo hadi hapo Mshtakiwa atakapopata nafuu ili kumpa fursa na haki ya kusikiliza kesi yake.
Kwa upande wake wakili wa utetezi, Ladislaus Lwekaza alikubaliana na maombi ya upande wa mashtaka na kwamba Serikali isimamie matibabu ya Mshtakiwa ili aweze kupata haki yake ya msingi ya kusikiliza kesi yake hata kama kuna wakili anayemwakilisha.
Kutokana na maombi hayo Hakimu Mteite aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 27, Mwaka huu itakaoondela kusikilizwa na kuagiza upande wa mashtaka kuhakikisha inawaleta mashahidi wote sita walionao.
Alisema siyo lazima mshtakiwa aweze kupona kabisa bali apate nafuu angalau ya kuweza kusikiliza kinachoendelea ili asije akatumia njia hiyo kuona kama kaonewa.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba F8302 wa Wilaya ya Mbeya ambaye kabla ya kufikishwa mahakamani alivuliwa Uaskari baada ya kuhukumiwa kijeshi.
Wengine kuwa ni mshtakiwa namba mbili kuwa ni, Askari Magereza mwenye namba B 500 Sajenti Juma Mussa(37) wa Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa Iyela na Amri Kihenya(38) Mkazi wa Iyela.
Awali Mwendesha mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe alisema washtakiwa wote kwa pamoja wanatuhumiwa kwa kosa moja la unyang’anyi wa kutumia Silaha kinyume cha Sheria kifungu cha 287 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3, Mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya Chunya.
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia gari aina ya Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo mawili ambayo ni GX 100 Toyota Cresta T 782 BEU na Gari linguine ambalo lilikuwa na namba za Chesesi GX 6011832 AINA YA Grand Mark II.
Awali kesi hiyo iliahirishwa kwa mara ya kwanza baada ya mshtakiwa kutofika mahakamani bila upande wa jamhuri kujulishwa hali ambayo Hakimu alimwagiza kufika mahakamani kwa njia yoyote hata kwa machela.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment