Mkurugenzi wa Shule ya Skondari ya Vanessa iliyopo Isyesye Jijini Mbeya, Shukrani Gidion akimkabidhi Godoro Aida Nakawala mama aliyejifunguwa watoto wanne |
Akikabidhiwa maziwa ya watoto |
Kushoto ndiye mume wa Aida yaani baba mzazi wa watoto watoto mapacha wanne |
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Vanessa iliyopo Isyesye Jijini Mbeya, Shukrani Gidion akiwa na watoto hao |
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya
Vanessa iliyopo Isyesye Jijini Mbeya, Shukrani Gidion, amempa msaada wa vitu
mbali mbali Mwanamke Aida Nakawala(25)aliyejifungua watoto wanne kwa mkupuo.
Akizungumza katika hafla ya kumkabidhi
msaada huo iliyofanyika katika Wadi la wazazi katika Hospitali ya Wazazi Meta
anakoendelea na matibabu, Mkurugenzi huyo alisema ni jambo la kushangaza kwa
binti mdogo kupata watoto wengi katika njia ya kawaida.
Alisema katika maisha yake ameishia
kusikia mapacha wawili au watatu lakini Mapacha Wanne imemshangaza sana jambo
lililomgusa kumsaidia baadhi ya vitu kulingana na mahitaji ya Mama Wanne ambaye
hata hivyo hali yake inaendelea vizuri pamoja na watoto wake.
Vitu alivyotoa ni pamoja na Godoro la
futi Tano kwa ajili ya malazi ya watoto baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali,
Blanketi, Shuka, Chandarua, Nguo za Mama, Mataulo ya Watoto pamoja na nguo
zake,Vifaa vya kunyonyeshea pamoja na Maziwa ya Watoto(lactojeni) ambavyo jumla
yake vikigharimu zaidi ya Shilingi Laki tano.
Mkurugenzi huyo awali aliongozana na
Waandishi wa Mtandao wa Mbeya yetu ambao mara kwa mara hujitolea kujua hali ya
mama huyo pamoja na watoto wake ambapo aliomba kusaidiwa kukabidhi msaada huo
ikiwa ni pamoja na kuzunguka madukani ambapo baadhi ya wauza maduka walionekana
kuguswa na kujitolea kwa namna mbili ikiwa ni kupunguza bei ya vitu na kutoa
nyongeza kwa ajili ya mama.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo hakuishia
hapo ambapo alichangia fedha ya mafuta kwa Mtandao wa Mbeya yetu uliojitolea
kumrudisha Mama huyo nyumbani kwake ambako ni umbali wa Kilomita 150 kutoka
Mbeya mjini.
Kwa mujibu wa taarifa za wauguzi katika
Hospitali ya Wazazi Meta wamesema hivi sasa Mama huyo hali yake ni nzuri na
anaweza kurudi kijijini kwao Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoani hapa kutokana na
watoto wake kuchangamka.
Aidha Mtandao wa www.mbeyayetu.blogspot.com
unaomba kwa Msamaria mwema yoyote atakayeguswa na jambo hili kuchangia fedha ya
mafuta kwa ajili ya kufanikisha safari ya mama huyo pamoja na Watoto wake ikiwa
ni pamoja na kuhakikisha mahali atakapoishi na watoto hao pana usalama gani.
Na Mbeya yetu
kwa mawasiliano
0754 374408
|
1 comment:
MWANAMKE HUYO ANAHITAJI MSAADA MKUBWA ZAIDI WA USHAURI WA KUFUNGA KIZAZI KWANI KWA MUJIBU WA HABARI, SASA ANA WATOTO SABA KATIKA UMRI HUO NA WOTE WAKO CHINI YA MIAKA KUMI.
Post a Comment