Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, May 1, 2013

SHIRIKA LA POSTA LAONYESHA UHAI WAO

LEONARD YEGELLA MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA POSTA AKIPOKEA ZAWADI YA MFANYAKAZI BORA TOKA KWA RAISI
MKOSA SHABANI MADANGANYA AKIPOKEA ZAWADI KUTOKA KWA MWAKILISHI WA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA KATIKA HAFLA ILIYOFANYKA KATIKA UKUMBI WA MKAPA JIJINI MBEYA
GENOVEVA ASSENGA KARANI WA SHIRIKA LA POSTA MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM NAYE AKIPOKEA TUZO YA MFANYAKAZI BORA
YEGELLA AKIPONGEZWA NA VIONGOZI WAKE
MAGRETH MABULA AKIPEWA ZAWADI YA MFANYAKAZI BORA KUTOKA SHIRIKA LA POSTA MKOA WA MBEYA
BAADHI YA WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA POSTA WAKISHANGILIA  KWA FURAHA
AFISA UHUSIANO WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA BWANA MIIGO AKIZUNGUMZA JAMBO WAKATI WA HAFLA YA KUWAPONGEZA WAFANYAKAZI BORA WA SHIRIKA HILO


MENEJA WA SHIRIKA LA POSTA MKOA WA MBEYA HASSAN MWANG'OMBE AKIZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI (HAWAPO PICHANI) KATIKA HAFLA YA KUWAPONGEZA WAFANYAKAZI WAO.
WATUMISHI wa Umma na sekta binafsi nchini wameaswa kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kuleta ufanisi katika kuziletea manufaa sekta wanazofanyia kazi.

  
Mwito huo umetolewa na baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la  Posta Tanzania ambao wametunukiwa Zawadi za wafanyakazi  bora kutokana na utendaji kazi wao baada ya kupigiwa kura na watumishi wenzao.


Wakizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na uongozi kwa wafanyakazi wote iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya baada ya kupewa nafasi ya kuwashukuru wenzao kwa kuwawezesha kuchaguliwa wafanyakazi bora wa Mwaka 2013.

  Leonard Yegella (Principal Finance Officer- usimamizi)ambaye pia alitunukiwa zawadi ya mfanyakazi bora na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete alisema anafurahia kupewa nafasi kama hiyo ambayo ameipata kutokana na ushirikiano mzuri na wafanya kazi wenzie.

  
Wengine waliotunukiwa zawadi na Uongozi wa Posta ni pamoja na Bi Genoveva G. Assenga karani wa Posta kutoka makao makuu Dar Es Salaam, Bi Magreth Mabula na Mkosa Shaban Madanganya walioibuka wafanyakazi bora kutoka Mkoa wa Mbeya.

No comments: