MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
ulioanzishwa Mwaka 1999 kutokana na Sheria ya Bunge kifungu namba 2 ya Mwaka
1999 inajivunia kuwa mfuko unaoongoza kwa kulipa mafao bora kwa watumishi na kwa wakati.
Wakizungumza na Mwandishi wetu wakati wa kilele
cha Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya walisema
pspf hutoa mafao bora zaidi katika sekta ya hifadhi ya jamii.
Walisema ubora wa shirika lao unatokana na mfumo wa kulipa mafao kwa wanachama
wake wastaafu kwa kutumia "pension factor" bora na mshahara wa mwisho
wa mfanyakazi tofauti na wastani wa mshahara unaotumiwa na taasisi nyingine za
hifadhi ya jamii.
Walisema
shirika lao linajivunia mafanikio mengi ikiwemo uwekezaji salama, unaozingatia
ukuaji wa thamani ya mfuko, maendeleo ya jamii na uwekezaji unao mgusa
mwanachama moja kwa moja. Mfuko katika kumuwezesha mwanachama kupata makazi
bora, unatoa mkopo wa nyumba kwa mwanachama aliyebakiza muda wa miaka mitano
kabla ya kustaafu kwa lazima na pia mfuko unatoa mkopo wa nyumba za gharama
nafuu kwa mwanachama yoyote ambaye amechangia kwenye mfuko kuanzia miaka
mitano.
wakieleza
mafanikio zaidi ya mfuko wao, wafanyakazi hao walisema mfuko umefanikiwa kukua
hadi kufikia thamani ya shilingi za kitanzania 1.2 Trillion hadi mwezi Machi
2013, ongezeko kubwa la wanachama hadi kufikia wanachama zaidi ya 340,000,
kutoa huduma bora kwa wanachama kwakuwa na ofisi mikoa yote ya Tanzania bara na
ulipaji wa mafao bora na kwa wakati.
Kwasasa
PSPF imeanzisha mpango wa uchangiaji wa hiari kwa wananchi wote walio katika
ajira rasmi na isiyo rasmi ambapo mwanachama ataweza kupata mafao mbalimbali
kama mafao ya elimu, ujasiriamali, kustaafu, kujitoa, ugonjwa na mirathi.
Uchangiaji unaanzia shilingi elfu kumi kwa mwezi na mwanachama yupo huru kuamua
namna yoyote ya uchangiaji na pia yupo huru kujitoa kwenye mfuko muda wowote
atakao uona ni muafaka.
Wakifafanua
zaidi kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba kwa wanachama, walisema hadi sasa zaidi
ya nyumba 600 zimejengwa na zipo tayari kwa kukopeshwa kwa wanachama wa mfuko
waliochangia kwenye mfuko kuanzia miaka mitano na kuendelea. Walitaja mikoa
ambayo tayari nyumba zimejengwa kuwa ni Dar es salaam, Mtwara, Tabora, Morogoro
na Shinyanga huku ujenzi ukitarajiwa/kuendelea katika mikoa ya Dodoma, Iringa,
Mbeya na Kilimanjaro. Ni mpango wa mfuko kujenga nyumba mikoa yote ya Tanzania
katika kuwahakikishia wanachama wake makazi bora.
PSPF
inawakaribisha wananchi wote ambao hawajajiunga na mfuko wowote wa hifadhi ya
jamii kujiunga nao.
|
No comments:
Post a Comment