Waheshimiwa madiwani wakiwa makini kumsikiliza mkurugenzi huyo
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wameshtukia mpango wa baadhi wa watumishi kuigeuza Halmashauri hiyo kama shamba la bibi kutokana na kukithili kwa vitendo vya ubadhilifu wa fedha ambavyo vimesababisha kushuka kwa ukusanyaji wa mapato kutoka Sh.Mil 600 zilizokusanywa mwaka jana katika kipindi cha miezi mitatu hadi kufikia Sh.Mil. 300 mwaka huu. Wakizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Rungwe Diwani wa Kata ya Masukulu, Rephson Mwaisupule, alisema kama vitendo vya ufujaji fedha vinavyofanywa na baadhi ya watendaji kama hali hii itaendelea Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Noel Mahyenga pamoja na Mweka Hazina wa Halmashauri, John Shirima wawajibike. Diwani wa Kata ya Masukulu, Rephson Mwaisupule, alisema miezi mitatu iliyopita katika kipindi cha mwaka jana fedha zilizokuwa zimekusanywa katika vyanzo vya ndani vya mapato zilikuwa Sh.Mil 600 lakini katika hali ya kushangaza mwaka huu zilizokusanywa ni Sh. mil. 300 tu. Diwani Robert Mwaibata alisema kupungua kwa ukusanyaji wa mapato hayo ni dhahili kwamba kumetokana na ufujaji wa fedha unaofanywa na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu ambao wamekuwa wakifoji stakabadhi za kukusanyia mapato. Akitoa maamuzi ya kikao cha kamati ya fedha mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe mheshimiwa Meckson Mwakipunga amesema kuwa hatua zimechukuliwa kwa kuwasimamisha kazi Watumishi 11 ili kupisha uchunguzi ufanyike. “Hatuwezi kukubali kuona Halmashauri inageuzwa shamba la bibi, madiwani lazima tuungane kuhakikisha tunawadhibi wafujaji wa mapato na kimsingi moto tulioanza kuuwasha mtaona wenyewe,”alisema Mwakipunga.
Na Ally Kingo Tky
|
No comments:
Post a Comment