Ikupa akiwa na mchumba wake Gervas siku ya send off huko Mwakaleli |
Wazazi wa Ikupa Dkt Akimu Mwalukosya pamoja na mkewe wakiingia kwenye sherehe ya kumuaga binti yao |
Ikupa akimkabidhi ua mchumba wake |
Bwana harusi mtarajiwa akiwa nyumbani kwao huko sae Mbeya akisubiria familia hizi mbili kukutana na kujuwa hatma ya ndoa yao |
Bwana harusi chanzo cha harusi kutofungwa kutokana na kutokuwa na mawasiliano mazuri na washenga wake ambao ni Bwana Amoni Mwangosi ambaye ni mshenga wa Bibi harusi na Bwana Angolile Mwakisilwa ambaye ni mshenga kwa upande wake wa Bwana harusi. Bwana harusi alitumia watu wengine kupeleka nauli ya sh 24,000/= ya kumchukua bi harusi na mpambe wake bila kufuata taratibu za kimira za kuwajulisha washenga wake ndiyo waende kumchukua mchumba wake hata hiyo watu hao walikataliwa kwa kutotambuliwa na familia hiyo ya bi harusi na kutaka wahusika wafike ili wakabidhiane kwa taratibu zinazotambulikana Kwa upande wake wa Mzazi wa Bibi harusi Mzee Akimu Mwalukosya, amesema hana kinyongo bali yaliyopita si ndwele na wagange yajayo kwani makosa yaliyofanyika yanazungumzika. Leo jioni kamati ya maandalizi upande wa bwana harusi wanakutana kujadili swala hilo Hata hivyo kamati ya sherehe ya bwana harusi itakutana kesho(jumatano) kupata hatima ya harusi hiyo. |
1 comment:
Mila hizi zilifaa enzi hizo hakuna magari. Watu walikuwa wanatembea kwa miguu. Sasa kwakuwa mila haziendi na wakati matokeo yake ndo haya!
Post a Comment