Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, November 8, 2011

Watendaji wa Serikali wametakiwa kutoridhika na taarifa za utekelezaji miradi mbalimbali - Mbeya

Na mwandishi wetu.
Watendaji wa Serikali wametakiwa kutoridhika na taarifa za utekelezaji miradi mbalimbali zinazotolewa na maafisa watendaji badala yake wametakiwa kufika maeneo husika kwa ajili ya kufanyia ukaguzi.

Tamko hilo limetolewa na kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mbeya Dokta Stephen Mwakajumulo wakati akiwa ziarani wilayani Chunya ambapo alipata taarifa ya kukamilika kwa mradi wa maji kata ya Mbuyuni na baada ya kutembelea eneo husika alikutana na taarifa iliyopishana ile aliyokabidhiwa kwenye maandishi.

Aidha akiwa kata ya Kanga dokta Mwakajumulo aliwataka watendaji kutojihusisha na mambo ya kisiasa na badala yake watumie muda wao kutekeleza majukumu yao kulingana na irani ya Chama kilichopo madarakani.

Naye diwani wa kata hiyo Enesi Shailosi amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wake amefanikiwa kumaliza mgogoro wa wafugaji na wakulima uliodumu kwa zaidi ya miaka 20 kwenye kata yake kwa kuwakutanisha pamoja na kukubalina namna ya ufanisi kufanya shughuli zao.

No comments: