Na mwandishi wetu
Mgogoro wa ardhi kati ya Bi.Sara Kalomba na uongozi wa kijiji cha Kongoro kata ya Kongoro Mswisi umeingia sura mpya baada ya mkuu wa wilaya Mbarali Kanali Kosimas Kayombo kudai kulifuatilia kwa ukaribu zaidi.
Hatua ya mkuu huyo wa wilaya Kanali Kayombo imekuja baada kupata taarifa kupitia kipindi cha Faster Faster kinachorushwa na redioo hii kuwa uongozi wa kijiji umeuza shamba Bi.Kalomba kwa siri na kudai kumtafutia shamba lingine katika sehemu nyingine.
Nao baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema kitendo hicho ni cha uonevu na kimelenga kuwanyanyasa walemavu kwa kufikiri kuwa hawajui chochote kuhusu sheria ya umiliki wa ardhi.
No comments:
Post a Comment