Sehemu ya mbele ya gari ikiwa imefunguliwa kwa uchunguzi zaidi
Picha chini :Askari polisi akilinda sehemu ya madawa ya kulevya yaliyotolewa kwenye gari hiyo
Kiwango kikubwa cha Madawa ya kulevya Kimekamatwa Hivi karibuni Tunduma zikitokea Mkoani Arusha zikiwa njiani kuvushwa kupelekwa Afrika ya kusini.
Watu wawili mwanamke na mwanaume walikamatwa akiwemo mwanamke Mzungu aliyejifungua greza la Ruanda Mbeya.
Madawa hayo ambayo yalikua yamefichwa kwenye sehemu mbalimbali za gari Dogo aina ya Pic Up Nissan Hard bord kama linavyoonekana ikiwa na namba za usajili za A.kusini inakadiriwa kati ya kilo 40 zilikamatwa.
TUKIO LA MZUNGU KUJIFUNGUA AKIWA GEREZANI. |
| |
RAIA wa Afrika kusini, Anastazia Cloete (26) mwenye asili ya Kizungu, aliyekamatwa mwaka jana katika mpaka wa Tanzania na Zambia, mji mdogo wa Tunduma amejifungua mtoto wa kike akiwa mahabusu kwenye Gereza la Ruanda jijini Mbeya akituhumiwa kukutwa na kilo 42.5 za dawa Za kulevya.
Cloete alijifungua mtoto wa kike miezi minne iliyopita baada ya kushikwa uchungu akiwa mahabusu na kukimbizwa katika hospitali ya wazazi ya Meta ambako alijifungua salama.
Cloete tayari alikuwa na ujauzito alipokamatwa na mumewe Vuyo Jack (30) na kujifungua salama, ingawa awali kulikuwa na wasiwasi wa kufanyiwa upasuaji.
Hata hivyo, inadaiwa mama huyo amekataa kumnyonyesha mtoto wake kwa madai kuwa hapati mlo wa kutosha unaomuwezesha kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mwanae.
Vuyo Emmanue Jack na Anastazia Elizabeth Cloete waliokuwa wakiishi mtaa wa 2A Valley Road-Schaapkraal-Capetown wanatuhumiwa kukutwa na kilo 42.5 za mihadarati novemba 18 mwaka jana katika mpaka wa Tunduma iliyofichwa kwenye gari aina ya Nissan Hard Body lenye namba za usajili CA-508-656, mali ya Vuyo Jack waliokuwa wakitokea mkoani Morogoro kuelekea Afrika Kusini.
Baadhi ya wanaharakati wa haki za binadamu waliohojiwa walidai kuwa kesi inayowahusu watuhumiwa hao inapaswa kuharakishwa ili mama na mtoto huyo waweze kujua hatima yao kuliko kukaa mahabusu muda mrefu na kuruhusu sheria ichukue mkondo wake ili kuona kama mama huyo alipokuwa mjamzito alikuwa akijihusisha na biashara hiyo.
Mchungaji William Mwamalanga alipohojiwa alisema haki ya mama na mtoto na haki za binadamu lazima zilindwe na akataka upelelezi uharakishwe.
DAWA HIZO ZA KULEVYA HIVI KARIBUNI ZILILETA UTATA NA KUSABABISHA VIGOGO WA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KUSIGANA.
SAKATA la upotevu wa kilo kadhaa za dawa za kulevya zilizokamatwa Novemba 18 mwaka JANA 2010 mkoani Mbeya, limechukua sura mpya baada ya vigogo watatu wa Jeshi la Polisi mkoani humo kung’olewa na wengine kuvuliwa vyeo.
Taarifa za uchunguzi na zilizothibitishwa na baadhi ya mamlaka na baadhi ya askari polisi, zimetanabaisha kuwa kati ya vigogo wa jeshi hilo waliosambaratishwa na kutarajiwa kuondolewa mkoani Mbeya hivi karibuni kuwa ni pamoja na kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi.
Vyanzo hivyo vya habari vilieleza kuwa mbali na kamanda huyo wa polisi wa mkoa wa Mbeya pia inadaiwa mkuu wa upelelezi wa polisi wa mkoa huo (RCO) Anacletus Malindisa na Staff One nao walitarajiwa kuondolewa mkoani Mbeya kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na tukio hilo la upotevu wa dawa za kulevya.
“Baada ya vyombo vya habari kufichua upotevu wa dawa za kulevya zilizokamatwa hivi karibuni mjini Tunduma na makao makuu kutuma kikosi cha uchunguzi sasa tayari kuna taarifa za uhakika za kuondolewa wakubwa hapa mkoani Mbeya huku baadhi wakihusishwa moja kwa moja na tukio hilo,’’ walisema baadhi ya maafisa wa polisi wanaofahamu kwa kina suala hilo.
Aidha vyanzo vingine vya ndani kutoka ndani ya jeshi hilo vimeeleza kuwa kamanda Advocate Nyombi anatarajiwa kuhamishiwa makao makuu ya polisi na kupangiwa kazi nyingine huku Malindisa akitarajiwa kuwa makamu wa RPC katika mkoa mwingine na Staff One akitarajia kuukwaa ukamanda wa polisi.
Hali hiyo haijawashtua askari wengi mkoani hapa kwa kile walichodai kuwa walitarajia tukio hilo kwani baadhi yao historia zao za kazi siyo nzuri sana.
Dawa zinazodaiwa kupotezwa kwa makusudi na kubadilishwa kuwa majivu kutoka mkoani Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam ni zile zilizokamatwa Novemba 18, 2010 mjini Tunduma zikiwa njiani kupelekwa nchini Afrika Kusini na watu wawili:
Vuyo Jack (29) na mwanamke mwenye asili ya Kiasia Anastacia Cloete (25).
Dawa hizo miongoni mwake kulikuwa kilo 1200 za heroine, Cocaine na Morphine zilizoingizwa nchini kupitia mpaka huo wa Tunduma kati ya Oktoba 27 – 30 mwaka huu. (Kwa hisani ya KALULUNGA NA PRESS NETWORK TANZANIA) |
|
No comments:
Post a Comment