Bi Sophia Masanja mkazi wa kijiji cha Ichesa, jimbo la Songwe wilayani Chunya mkoani Mbeya akichota maji kwenye chemchem kutokana na uhaba wa maji kijijini hapo, ambapo hulazimika kuamka saa 11 alfajiri kusubiria maji kujaa toka kwenye mfereji wa Chemchem. Mkazi huyo alikutwa na mpiga picha wetu juzi Jumapili.
Watanzania tukiwa katika hekaheka za kusheherekea miaka 50 ya Uhuru wananchi wengine vijijini hawana Maji. Pichani wakazi kijiji cha Ichesa, jimbo la Songwe wilayani Chunya mkoani Mbeya wakisubiri kuchota maji kwenye chemchem mojawapo juzi Jumapili ambayo hutiririsha maji kijijini humo.Wananchi hao hulazimika kuamka saa 11 alfajiri kila siku kusubiri Chemchem hiyo kujaa maji.
No comments:
Post a Comment