Meneja uzalishaji wa Kapunga Rice Project Bwana SERGEI BEKKER akielezea ramani ya Mashamba ya Kapunga.
*****
Na mwandishi wetu.
Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka mwekezaji wa shamba la Kapunga lililopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya kufungua njia aliyoiziba ndani ya siku 30 na kuongeza kuwa endapo asipotekeleza watatumia nguvu ya umma kuifungua njia hiyo.
Tamko hilo wamelitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Akiongea kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya mjini John Mwambigija amesema wakazi wa kijiji hicho wanasababu ya kumpinga mwekezaji kutokana na kushindwa kuwa na uhusiano mzuri na majirani zake.
Nao wananchi waliohudhuria mkutano huo waliunga kauli zilizotolewa na CHADEMA kwa kusema kuwa wako tayari kufanya maandamano ili kudai haki yao.
Naye aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CHADEMA jimboni humo katika uchaguzi uliopita bwana Kazamoyo Jidawa amesema kuwa inasikitisha kuona wananchi wazawa wakiishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao huku Mwekezaji akifanya atakavyo katika ardhi yao.
No comments:
Post a Comment