Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, October 18, 2011

SERIKALI MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI YAINGILIA KUCHUNGUZA SAKATA LA MGOGORO KATI YA FAMILIA YA OCS NA MWANANCHI.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama.
*****
Na mwandishi wetu

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Evansi Balama amesema Serikali kwa kushirikiana na Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi wa mgogoro kati ya familia ya OCS wa Trafiki Henry na Marry Msigalo na kuongeza kuwa mke wa askari huyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.



Ameyasema hayo katika mahojiano na mwandishi wetu kuhusu msaada wa Serikali katika mgogoro wa mda mrefu unaohusisha familia ya askari na raia ambapo mke wa askari huyo anadaiwa kutumia cheo cha mumewe kuwanyanyasa raia sanjari na kuharibu mali zao huku akitumia kikundi cha vijana.



Awali wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya wakazi wa kata Iganzo wamesema kwa kipindi cha miaka miwili wamekuwa wakipatwa na usumbufu kutoka kwa familia ya askari huyo na kila wanapojaribu kulizungumzia hilo Askari Henry anasema hawezi kutumia muda wake kujadili mambo yanayohusu wanawake kama wanavyosema.



Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipoulizwa kuhusu suala hilo ameahidi kulitolea ufafanuzi baada ya uchunguzi kukamilika.

1 comment:

Anonymous said...

asante Balama tuokoe na hilii