Mkuu wa wilaya ya Chunya Mheshimiwa Deodatus Kinawiro.
*****
Na mwandishi wetu.
Bi.Winfrida Mapunda mkazi wa Lupa wilayani Chunya anayekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 66 hadi 68 amenusurika kifo wakati akiwa njiani kwenda kuchota maji baada ya kuvamiwa na chui.
Bibi huyo amesema kwamba septemba 27 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili za asubuhi akiwa anaelekea kisimani kuchota maji alivamiwa na Chui kisha kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake.
Ndugu wa bibi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Chiristina Sijaona amesema muda mchache mara baada ya bibi huyo kuvamiwa na Chui raia wema walifika eneo la tukio na kuanza kumshambulia chui huyo kwa silaha za jadi hadi kumuua.
Aidha Bi.Sijaona ameiomba Serikali na wasamalia wema kutoa msada wao wa kiasi chochote ili kumsaidia bibi huyo kupata matibabu kwa urahisi kutokana na familia hiyo kutopewa msaada wowote kutoka Serikalini licha uongozi wa mali asili na utalii kutoa ahadi ya kugharamia matibabu ya bibi huyo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Chunya Deogratusi Kinawiro amekiri kupata taarifa za mtu kujeruhiwa na chui na kuongeza kuwa chui huyo aliuawa na wananchi na kwamba walikuwa chui wawili ambao walikuwa wametokea kwenye mbuga inayosadikiwa ni ya Katavi.
No comments:
Post a Comment